
KARIBU msomaji wangu. Tuendelee kutoka pale tulipoishia waki iliyopita.
Ni jambo la muhimu kujua namna ya kuepuka mawazo ya kile ambacho mwenzi wako amekutenda. Ulishaamua, kwa hiyo hutakiwi kukumbuka chochote. Pendelea kuwa huru, njia sahihi ni kupiga hatua bila kukumbuka mawazo machafu ya kutendwa ambayo yatakurejesha kwenye maumivu.
ZIFUNDISHE FIKRA ZAKO KUYAWEKA MBALI MAUMIVU
Kama utaweza kujua misingi ya kibaiolojia na kisaikolojia ya hisia hasi, hapo itakuwa rahisi kwako kujifunza jinsi ya kudhibiti maumivu ya kihisia, kwa hiyo utaweza kuyaondoa. Kama upo katikati ya wingu la maumivu, kabla hujafanya chochote, hakikisha umeondosha hicho kiwingu.
Ni jambo la muhimu kujua namna ya kuepuka mawazo ya kile ambacho mwenzi wako amekutenda. Ulishaamua, kwa hiyo hutakiwi kukumbuka chochote. Pendelea kuwa huru, njia sahihi ni kupiga hatua bila kukumbuka mawazo machafu ya kutendwa ambayo yatakurejesha kwenye maumivu.
ZIFUNDISHE FIKRA ZAKO KUYAWEKA MBALI MAUMIVU
Kama utaweza kujua misingi ya kibaiolojia na kisaikolojia ya hisia hasi, hapo itakuwa rahisi kwako kujifunza jinsi ya kudhibiti maumivu ya kihisia, kwa hiyo utaweza kuyaondoa. Kama upo katikati ya wingu la maumivu, kabla hujafanya chochote, hakikisha umeondosha hicho kiwingu.
Mambo yako hayatakwenda kama unavyotaka ikiwa wewe mwenyewe utashindwa kudhibiti na kuondoa. Hivyo basi, unatakiwa ujifunze na uielekeze akili na fikra zako kuyaweka mbali maumivu kabla ya kuyapuuza na kuyasahau moja kwa moja.
Pointi muhimu ya kuifanya akili na fikra zako kuyaweka mbali maumivu ni kuheshimu matarajio yako. Una mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha maendeleo yako ya kimaisha na kimapenzi. Hayo hayawezi kutimia kama utakuwa unaishi na mzigo wa kumbukumbu za kutendwa.
Mwenzi wako alikuumiza, hiyo sawa, lakini maisha hayapo tambarare. Kuna baya la leo na zuri la leo. Hivyo hivyo, lipo zuri la leo na baya la kesho. Mtu mbaya leo anaweza kuwa mwema kesho. Zingatia hilo, kwa mantiki hiyo hutakiwi kuishi ukiamini unaye adui wa kudumu. Mungu ndiye anaijua kesho.
Uzoefu unaonesha kuwa watu wengi wanaoishi na maumivu ya kutendwa na wenzi wao na wakashindwa kuyasahau, maisha yao ya kimapenzi huwa siyo mazuri. Huishi kwa kinyongo na mara nyingi ni wepesi kulaumu na kutoa kauli za kutaka waonewe huruma.
Mwenzi wako amekusaliti na imekuuma, chukua uamuzi na uendelee mbele. Ukimsamehe iwe ni uamuzi toka moyoni na ukiona hakufai tena, hiyo ibaki historia. Ni kwa nini upoteze muda wako kufikiria tendo lililopita? Ukiweza, kumbuka mazuri yenye kukupa faraja, mabaya usiyape nafasi.
ELEWA TABIA ZA MWENZI WAKO
Maisha yako yatakuwa rahisi kama utazielewa tabia za mwenzi wako. Hii inamaana kuwa ni kosa kubwa kuangukia kwenye mapenzi na mtu ambaye hujamsoma na humjui kwa undani. Kuishi na mtu ambaye humjui ni sawa na kubeba mzigo mzito kichwani ambao ndani yake hujui kuna nini.
Mchunguze mwenzi wako. Muelewe kinaga ubaga na baada ya hapo hatakusumbua tena. Ni mjivuni, mbinafsi, hilo unalitambua kikamilifu, kwa hiyo anajinunulia mavazi yeye mwenyewe bila kukununulia na wewe, haitakusumbua. Unamjua, ndiyo tabia yake.
Kama ni msaliti, umemsoma na umegundua ana tabia ya kuruka ruka nje. Baada ya hapo, ni nafasi yako kupima kama unaweza kumvumilia au uendelee mbele na maisha yako. Kama umeona ugandane naye, hii inamaanisha kuwa siku ukiona SMS za ajabu kwenye simu yake hutashtuka sana.
Si unamjua? Kigeni kipi? Hii ndiyo mantiki ya kukutaka umsome vilivyo mwandani wako. Usimbebe kama biashara ya kuuziana mbuzi kwenye gunia. Jipe kazi ya kumchunguza kwa makini. Amini kwamba ukishamtambua inavyotakiwa, utapumua.
Umeshawahi kusafiri kwa miguu umbali mrefu ambao hujui mwisho wake ni wapi? Unaweza kuhisi usumbufu wa kimawazo, akili na hisia kutokana na kushindwa kuelewa mwisho wa safari? Basi hali hiyo ni sawa na kuwa na mpenzi ambaye humjui kwa undani.
Ukishamjua kwa undani hatakusumbua. Itakuwa rahisi kudhibiti maumivu ya kiakili na moyo ambayo unaweza kuyapata kwa sababu yake. Itakuwia rahisi kuifundisha akili yako kuyaweka mbali maumivu ambayo atakusababishia, kwa hiyo maisha
yako yataendelea kuwa mazuri hata baada ya yeye kukusaliti.
No comments:
Post a Comment