Advertisements

Tuesday, July 31, 2012

WAGOSI WA KAYA MPO

Jumba la sinema lililopo Silver Spring, Maryland lenye jina Majestic ambalo lilikua maarufu Mkoni Tanga

MPAMBANO WA NGUMIIBF AFRICA KUTIKISA IDI PILI DIAMOND JUBILEE

UKISHIKWA SHIKAMANA


MR AND MRS EMMANUEL MSANGI WA CHICAGO IL AKIWA NA FAMILIA YAKE MBELE YA UKODAK WA VIJIMAMBO


SAKATA LA USAJILI WA NGASSA - SIMBA WATUMA OFA YA MIL.25, YANGA MIL.20: NGASSA ASEMA ATACHEZA POPOTE ATAKAPORIDHIKA NAPO



Siku moja baada ya klabu ya Azam kutangaza kumuweka sokoni Mrisho Khalfan Ngassa kwa ada ya uhamisho wa $50,000, kulwa na doto wa soka la Tanzania vilabu vikongwe Simba na Yanga vimetuma ofa rasmi ya kutaka kumsaini mshambuliaji ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Azam kupitia mtandao wake rasmi hadi sasa klabu ya Simba imetuma ofa ya shilingi millioni 25 na Yanga wametuma millioni 20.

Taarifa hiyo ilisomeka: "Hadi hivi sasa Ofa ya Simba ni shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20. kutokana na hilo. Simba wapo kwenye nafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya Mwisho. Ingawa tungependa kumuuza Mrisho Ngasa Yanga lakini tutampeleka kwa timu iliyotoa ofa nzuri zaidi
Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu ambayo atacheza kwa raha na amani, kutokana na yeye kuivaa na kuibusu Jezi ya Yanga siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga... Azam FC inaamini kuwa Yanga ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho, lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa na haja na Mrisho na ndiyo maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana. Kutokana na sababu hizo Azam FC italazimika kumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani hatuhitaji kuwa na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand ya Azam FC ambayo tunajaribu kuijenga."
Baada ya kutoka kwa taarifa tuliwasiliana na mchezaji mwenyewe Mrisho Ngassa kuzungumzia suala la uhamisho wake alisema: "Mimi nina mkataba na Azam na wao ndio wana maamuzi dhidi yangu. Kama wameamua kuniuza mie sina tatizo. I am proffesional footballer, hii ndio kazi yangu na nitaifanya popote nitakaporidhika napo."


By Aidan Charlie

DITTO APATA PIGO KWA KUONDOKEWA NA BABA YAKE MZAZI



Ditto msanii kutoka THT, usiku huu majira ya saa moja usiku ameondokewa na baba yake mzazi anayeitwa Lambert Tido. Ditto anasema baba yake alikuwa akisumbuliwa na Figo kwa mda mrefu hadi mauti yalipomkuta usiku huu katika hospital ya Taifa Mwimbili
Bongo Star Link inakupa pole sana Ditto na mungu akupe nguvu nyingi kwenye kipindi hiki kigumu ulichokuwa nao.

MATUKIO KATIKA PICHA NDANI YA CHICAGO NA BANG PARTY

 Chicago down town inavyoonekana kwambali kupitia lake Michigan, unaweza kufikiria ni bahari him kumbe ni ziwa mambo ya vijimambo hayo.
 Wakazi Wassira Kushoto na Dulla Solo wakipeana challenge ya mistari ya hip pop Wakazi ni mwanamuziki kizazi kipya and Dulla Solo ni Tanzania hip pop legend.
 Dulla Solo akiwa na Stanboi aka the Afican Child, Stanboi  mwanamuzik wa kizazi wa r&b na kwa sasa anatamba na kibao chake cha feel good akipata ukodak na legend wa hip pop
Stanboi na nembo ya Tshirt zake zinazo julikana kama the African child akiwa na watu walio walionunua kutoka kwake.

Ukodak wa vijimambo watu wakishow love mwanzo kushoto mdau wa Chicago kati ni Stanboi kutoka    Wichita Ks na Dr Kally kutoka Detroit MI Dr Kally ni jina la kisanihi nae licha ya kufanya kazi za kuajiliwa pia ujiusisha na muzik wa hip pop pale anavyo pata muda.
Pita pita ya camera ya vijimambo ikakuta parking hii hipo full na vyombo vya majini katika lake Michigani Chicago..........kama unavyo jionea.

RAIS KIKWETE AFUTURISHA MKOANI LINDI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru waalikwa kwa kuhudhuria kwenye hafla ya futari aliyoandaa katika Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi jana Julai 30, 2012.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Ludovick Mwananzila akishiriki katika futari hiyo pamoja na waalikwa wengine.
Waalikwa wakipakua futari.
Kadhi wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Shekhe Mkuu wa Mkoa Mohamed Saidi Mushangani akitoa neno la shukurani baada ya futari.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wageni waalikwa baada ya kufuturu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Lindi (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Uhamiaji ya mkoa waliokuwa miongoni mwa wageni waalikwa.
(PICHA NA IKULU)

UZINDUZI WA KITABU NA SEMINA HOLIDAY INN HOTEL THIS SUNDAY


HAYA NDIO MAGOLI YA YANGA - WALIPOITANDIKA AZAM KATIKA KAGAME CUP



YANGA WALIVYOTWAA UBINGWA WA KAGAME 2012.


Picha ya pamoja
Kikosi cha timu ya Yanga
Mshambuliaji wa timu ya Yanga akishangilia na Kombe mara baada ya timu yao kutwaa Ubingwa wa ligi ya Kagame
Mkuu wa Mkoa akikagua timu za Azam na Yanga wakati wa fainali ya Ligi ya Kagame
Picha ya pamoja ya Yanga, Azam na Mgeni rasmi
Kikosi cha timu ya Azam
Mshambuliaji wa timu ya Yanga akishangilia mara baada ya kuipatia timu yake ya Yanga goli la kwanza
Mashabiki wa Yanga wakishangilia

Sheria mpya ya madaktari yaja


Serikali inakusudia kutunga sheria mpya ya madaktari, kutengeneza kanuni za kuwasilisha malalamiko dhidi ya wanataaluma wa afya pamoja na kupitia na kusambaza miiko na maadili ya taaluma ya udaktari.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, aliliambia Bunge jana mjini hapa alipokuwa akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwama 2012/13.

Alisema wizara yake itaandaa nyaraka mbalimbali za Baraza la Mawaziri ili kuwasilisha serikalini na katika ngazi mbalimbali zinazohusiana na kada hiyo kwa ajili ya kutekeleza azma ya kutunga sheria ya madaktari.

"Wizara itaandaa nyaraka na kuziwasilisha katika ngazi husika kwa ajili ya maamuzi, mapendekezo ya miswada ya kutunga sheria mpya ya madaktari na madaktari wa meno," alisema.

Dk. Mwinyi alisema kazi ya kutengeneza kanuni za kuwasilisha malalamiko dhidi ya watumishi wa kada ya afya itafanywa na Baraza la Madaktari Tanganyika ambalo pia litapitia na kusambaza miiko na maadili ya taaluma ya udaktari.

Alisema baraza hilo pia kwa kushirikiana na wizara yake litafanya ukaguzi wa hospitali zinazofundisha mafunzo kwa vitendo na zile za rufaa za mikoa ili kuangalia ubora wake.

Alisema lengo nikubaini idadi ya hospitali zitakazohimili idadi ya madaktari wanaohitimu vyuo vikuu.

Alisema nyaraka nyingine zitakazoandaliwa ni za kupendekeza kutungwa kwa sheria mpya ya wazee, kufanya mabadiliko ya sheria ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) sura ya 150, marekebisho ya sheria iliyoanzisha Taasisi ya Chakula na Lishe, sheria ya kuwianisha mfuko wa afya vijijini (CHF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na kufanya mabadiliko ya sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219.

Azam yamuuza Ngassa milioni 80/-

Uongozi wa klabu ya Azam ya jijini Dar es Salaam umesema kuwa umekasirishwa na kitendo cha kuibusu nembo ya klabu ya Yanga kilichoonyeshwa na mshambuliaji wake Mrisho Ngassa na kuongeza kwamba sasa uko tayari kumuuza mchezaji huyo kwa dola za Marekani 50,000 (Sh. milioni 80).

Hatua hiyo ya Azam imekuja kufuatia nyota huyo kuonyesha wazi mapenzi yake kwa klabu yake hiyo ya zamani, ambayo ni bingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati.

CCM YAMSHUKIA TUNDU LISU

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari, leo, Julai 30, 2012, katika ukumbi wa Sekretarieti,. Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
  • Yadai orodha yake inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
  • Anataka kuwaokoa wa Chadema katika sakata hilo.
  • Yasema tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe la kisiasa
NA MWANDISHI WETU
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

Lissu awalipua wabunge saba *Adai ndio wanahusika na kashfa ya rushwa *Yumo Ole Sendeka, Vicky Kamata, Nassir

Na Benedict Kaguo, Dodoma

MNADHIMU wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Bw. Tundu Lissu, jana amewataja kwa majina wabunge saba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anodai kuhusika na kashfa za rushwa ambayo inalihusu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Bw. Lissu aliwataja wabunge hao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Hatua hiyo imekuja wakati ambao wabunge, wanasiasa, wananchi na  wanaharakati wakiwa na shauku ya kutaka kuwajua wabunge ambao wanatuhumiwa kwa kashfa hiyo.

Katika kikao hicho, Bw. Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashiriki (CHADEMA), bila ya kuuma maneno, alisema wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya rushwa ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini (iliyovunjwa na Spika Bi. Anne Makinda).

Aliwataja wajumbe hao kuwa ni Bw.  Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Bi. Sara Msafiri (Viti Maalum), Bi. Mariam Kisangi (Viti Maalum), Bw. Yusuph Nassir (Korogwe Mjini), Bw. Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) Bi. Vicky Kamata (Viti Maalum) na Bi. Munde Tambwe (Viti Maalum).


Alisema hadi sasa, kambi ya upinzani ina ushahidi juu ya ushiriki wa wabunge hao katika kashfa hiyo na kutaka wachukuliwe hatua.

Aliongeza kuwa, wajumbe wengine wa kamati hiyo kutoka CHADEMA, Bw. John Mnyika (Ubungo), Bw. David Silinde (Mbozi Magharibi) na Mwanamrisho Taratibu Abama (Viti Maalum), hawahusiki kabisa katika kashfa hiyo.

Alisema Bi. Msafiri na Bi. Tambwe, wamekuwa wakipewa tenda ya kuiuzia matairi TANESCO huku wakijua wao ni wajumbe wa kamati hiyo ambapo Bw. Mwijage, amekuwa akifanya kazi ya Mtaalamu Mwelekezi wa Kampuni ya Puma Energy.

Bw. Lissu alisema, kampuni hiyo nayo imeingia katika mgongano wa kimasilahi na kampuni nyingine ambapo Bw. Nassir na Bi. Kisangi, wanamiliki vituo vya mafuta hivyo wana mgongano wa kimasilahi ndani ya Wizara hiyo.

Akimzungumzia Bw. Ole Sendeka, alisema mbunge huyo hana kituo cha mafuta wala mgongano wa kimasilahi bali amekuwa mtetezi mkubwa wa Kampuni ya Orxy na Camel.

Alisema kampuni hizo zimekosa tenda ya kuizuia mafuta IPTL, huku akimtaja Bi. Kamata na kudai kuwa, mbunge huyo hana mgongano wa kimasilahi ila ana masilahi binafsi.

Hata hivyo, Bw. Lissu alisema wabunge hao wamejihusisha na vitendo ambavyo ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995, inayokataza kuwepo migongano ya kimasilahi.

UJUMBE WA WANAFUNZI

Wapendekeza Katiba Mpya ifute Muungano-Mwananchi

MUUNDO wa  sasa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,unapaswa kufanyiwa marekebisho kupitia Katiba Mpya, ili kupunguza manung’uniko na hatimaye mwafaka kuhusu Muungano.
Hayo yalisemwa juzi na wananchi wa Jiji la Tanga, walipokuwa wakitoa maoni yao kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Mabadiliko ya Katiba Mpya.

Wananchi hao, wamedai kuwa muundo wa sasa wa Muungano hauna tofauti na kuwaunganisha tembo na sungura, jambo ambalo haliletin usawa.

DICOTA 2012 CONVENTION - AUGUST 30 - SEPTEMBER 2,2012


Dear MEMBERS OF DICOTA and FRIENDS:
You are invited to attend the DICOTA 2012 Convention – themed “Tanzania’s Diaspora - Investment, Citizenship and Relationship” – to be held at the Chicago Marriott O'Hare, 8535 West Higgins Road · Chicago, Illinois 60631 U.S.A. from 30th August to 2nd September, 2012.


The former President of Zanzibar, H.E Aman Abeid Karume is the invited Guest of Honor


The convention brings together members of the Tanzanian Diaspora in the United States America, Tanzanian private sector and government officials; key decision makers from Tanzania and U.S. businesses; financial institutions, and international organizations with vested interest in investment and growth in the country. The conference presents attendees with the latest trade and investment opportunities in all sectors of the economy, while providing a forum for potential partnership formation through many networking opportunities.
This year we will have a very important session to discuss about our inputs to the Commission which is reforming Tanzanian Constitution. Come and make your views heard and be part of this important milestone in our History.

Please make time and Plan to attend this Extra-Ordinary Convention. Click here to register, early Registration with Great discount Ends August 16, 2012. For more Information about Convention Registration, Hotel Discount Rates and Program visit us at www.dicotaus.org. You can also contact us by emailconvention@dicotaus.org or call 1-952-217-0265 to reach a convention steering committee representative.

Sincerely,
Dr. Ndaga Mwakabuta,
DICOTA - President

FUTARI YA PAMOJA


FUTARI YA PAMOJA
WASHINGTON DC
Kwaniaba ya Chama Cha Mapinduzi, Mwenyeki na Uongozi wa CCM Tawi la DMV tunawatakia waislam wote duniani Ramadhani njema.
Pia Tunawakaribisha watu wote katika futari ya pamoja
Kama ilivyo desturi tunaungana nao katika mwezi huu wa Ramadhani.
Watanzania wote mnakaribiswa katika futari hiyo  ya pamoja.

SIKU:   IJUMAA: AUGUST 3, 2012
WAKATI: 7.30 P.M.
ADDRESS: 10615 New Hampshire Avenue
                   Silver spring, MD 20903

RAMADHANI KAREEM
UONGOZI WA TAWI

FURSA KWA VIJANA WA DODOMA WIKI IJAYO

Habari
Mimi ni mjasiriamali na mwezeshaji na kocha wa biashara,Kwa kifupi tu Naitwa Deogratius Kilawe.Wiki ijayo nitakuwepo Dodoma,natafuta wawakilishi au wanafunzi wa dodoma university,hombolo na vyuo vingine kama CBE,ST.JOHN ili nikija huko next week nifanye semina mbili tatu kama wewe unatoka vyuo vya dodoma wasiliana nami sasa ili nije nifanye semina ya FURSA ZILIZOPO TANZANIA ZINAZOWEZA KUKUSTAWISHA KIBIASHARA. Piga simu namba 0717109362 kuwasiliana nami.Pia nitakuja na vitabu vyangu na kuteua agent wangu wa vitabu vyangu.
Pia Taasisi nyingine za mambo ya biashra tunaweza wasiliana.

Piga 0717109362


DJ Babu & Kaka: Get Well Fundraiser


20120727104308-babukaka1
DJ Babu & Kaka were victims of a near death car accident that put them in the ICU. Let's help them raise money during recovery
Hello, my name DJ Fully Focus & my two long time friends & business partners DJ Babu & Kaka of the TakeOverDJs entertainment crew were victims of a near death car accident in Delaware that left them both in the ICU on Tuesday, July 17th, 2012. They were travelling back to DC when they pulled off on the side of the highway to fasten sound equipment which they had just purchased, when another car travelling on the highway lost control & veered off the highway striking both their bodies directly as well as the car.
The near fatal accident left both them in the E.R. with broken bones, Babu (broken leg & shoulder) Kaka (broken leg, collar bone & ribs) not to mention trauma. Since then they both have undergone successful surgeries but both are still in the hospital (Christina Hospital Trauma Center in Delaware) though Kaka is still in the ICU as he suffered more severe impact.
All of the contributions given will help with whatever expenses their families might need to sustain them throughout their stay in the hospital and during their recovery. Our goal is $10,000 as we want to be able to provide enough money for both Babu & Kaka and their families so they won’t have to worry about bills during this difficult time. Babu's sisters & mother (who reside in New Jersey) & Kaka's wife (residing in Maryland) have taken time off work since the incident took place to travel & be with their loved ones. The duration for recovery is said to be 12+ weeks (which also means no work/events/income during this time). We want to be able to insure that both Babu & Kaka will be with their families during this difficult time and not have to worry about lack of funds. Should we not reach our goal of $10,000, that’s ok because anything helps at this point!
Please share & help us spread the word by all means.

$600
Raised of $10,000 Goal
32 days left

Flexible Funding campaign

This campaign will receive all of the funds contributed by Fri Aug 31 at 11:59PM PT.
-TakeOverDJs

Ulimboka ‘atikisa’ Bunge


Kizitto Noya, Dodoma
SAKATA la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, limeibuka upya bungeni baada ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kuitaka Serikali itoe majibu ya kina kuhusu watendaji wake kutajwa kuhusikana na tukio hilo.


Kambi hiyo pia imeitaka Serikali ieleze sababu za watendaji hao kutokamatwa hadu sasa na kuhojiwa na vyombo vya dola, wakati kuna taarifa kuwa wanafahamika.

Mtikisiko


Wanafunzi wa shule za Msingi za Temeke wakiingia kwenye ofisi za Manispaa ya Temeke kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana na kuwasababishia kukosa masomo.Picha na Elizabeth Edward
WALIMU WAGOMA KILA KONA, WANAFUNZI NAO WACHACHAMAA, SERIKALI YAONYA, YATISHIA KUWAFUTIA MISHAHARA 
Waandishi Wetu
NCHI imetikiswa. Mgomo wa walimu ulioanza jana katika sehemu mbalimbali nchini, umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu huku kukiwa na taarifa za matukio yasiyokuwa ya kawaida yaliyoambatana na mgomo huo usio na ukomo.

Katika sehemu mbalimbali nchini, walimu waliripotiwa kugoma kwa kutoingia madarasani na wengine walifika kazini na kusaini vitabu vya mahudhurio kisha kuondoka hali iliyosababisha wanafunzi kurandaranda ovyo katika sehemu za miji iliyo karibu na shule hizo.

Mjini Dodoma ,wabunge jana walimbana Naibu Spika, Job Ndugai wakitaka shughuli za Bunge zisitishwe ili kujadili mgomo wa walimu ambao umeanza rasmi jana nchi nzima, na kuziacha shule nyingi zikiwa na walimu wakuu na wakuu wa shule pekee.

Gangamala, usiuze mechi, ni kosa kusema umechoka faragha!-3


UTAPOTEZA MVUTO WAKO
Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii inamaana ya kuongeza mvuto!
Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia.

Monday, July 30, 2012

ZITO AHOJIWA KWA RUSHWA

SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

BONDIA IBRAHIMU CLASS AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WA IDI PILI

Bondia Ibrahimu Class kulia akipambana na Whence Haluni 'West Scopion' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ilala Dar es salaam Class anajitarisha na mpambano wake na Simba Watundulu litakalofanyika Sikukuu ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee Bondia huyo ambaye yupo chini ya Makocha Habbu Kinyogoli pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' anategemea kuonesha ufundi wa ali ya juu katika mchezo wa masumbwi nchini. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

WANACHAMA WAPYA WALIOJIUNGA CCM DMV

 Wanachama wapya DMV wajiunga na Chama Cha Mapinduzi kushoto ni Dedy Luba na Dj Seif
Wanachama wapya wakiwa na Mwenyekiti Loveness Mamuya ( wapili toka kushoto) na katibu CCM DMV Jacob Kinyemi ( wakwanza kulia)

IN EVERLOVING MEMORY OF OUR BELOVED


MACRINA JOSEPH SAMAKA

It is one year today since you departed from our midst to be with the Lord on July 31, 2011. The heartbreak and pain that we felt has not and will never cease. However, God continues to be our refuge and inspiration. Your precious memories remain fresh in our hearts and minds. The love you placed within our hearts no millionaire could buy.

You are fondly remembered by your loving father, brothers, sisters, nephews, your lovely niece, brother-in-law, relatives, neighbours and friends. We will always remember you.

There will be a memorial mass for the departed soul at the Msimbazi Catholic Church on Saturday, August 4, 2012 at 6:45 am. All are welcome.

MAY THE ALMIGHTY GOD REST HER SOUL IN ETERNAL PEACE, AMEN 

"DREAM and YOUR INTERNAL CAPACITY"-BY MWL.MWAKASEGE


Mtumishi wa Bwana,
Bwana Yesu Kristo Apewe Sifa,
Huduma ya Mana-Ministries USA inapenda kupanda mbegu ya mafundisho kwenye maisha yako ambayo yamefundishwa live na mtumishi wa Mungu Mwl.Mwakasege July 21 2012 kupitia Tele-seminar.
Tumepokea shuhuda nyingi jinsi ambavyo wengi wamefunguliwa na kuponywa na mafundisho haya.Ndoto [dreams] za wengi tayari zimefufuka kupitia semina hii.
 
Tunalokuomba wewe unayepokea ujumbe huu ni kuendelea kuombea watumishi hawa Diana na Christopher Mwakasege pamoja na huduma hii ya Mana.
 
Pili,tunakusihi uwatumie watu wengine ujumbe huu muhimu.Huwezi kujua nani atasaidika kiasi gani na mafundisho haya. Majibu ya maombi ya wengine yamo ktk ujumbe huu.
 
Ubarikiwe sana na usikose Tele-Semina nyingine ya Mwezi August 2012.
 
Mana-Ministries (USA).



CHEKA UNENEPE

HAPPY BIRTHDAY ZAY B

 May almightys best blessings showered on your Happy Birthday Zay B

CCM NA CHADEMA ZATANGAZA KIAMA KWA WABUNGE MAFISADI



VYAMA vya CCM na Chadema vimetoa onyo kali kwa wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuhongwa na baadhi ya kampuni za mafuta na kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikisema havitasita kuwawajibisha pindi tuhuma hizo zitakapothibitika.
Kauli ya vyama hivyo imekuja siku moja baada ya wabunge watano, watatu wa CCM na wawili wa upinzani kudaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa, ambavyo vimesababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili majina ya wahusika yawekwe hadharani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa vyama hivyo walisema wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka bungeni.
CCM: Rushwa adui wa haki
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema chama hicho kimewaapiza wanachama wake wote kutotoa wala kupokea rushwa.

Dk Kawambwa: Mawaziri wasiwe wabunge


Editha Majura, Bagamoyo na Fidelis Butahe, Dodoma
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema utaratibu wa sasa wa mbunge kuwa waziri haufai na badala yake amependekeza Katiba Mpya itamke kuwa atatoka nje ya Bunge.
Hii ni kauli ya kwanza katika siku za hivi karibuni kutolewa na waziri ambaye yupo katika Serikali iliyopo madarakani.
Dk Kawambwa alisema hayo jana wakati akitoa maoni yake kama raia kwenye Kituo cha Vigwaza, Pwani wakati Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipokuwa ikichukua maoni ya wananchi.
Baada ya kutoa maoni yake, Mjumbe wa Tume hiyo, Ally Salehe alitaka kujua msimamo wa Dk Kawambwa kuhusu mbunge kuteuliwa kuwa waziri jambo linalipingwa na watu wengi.
“Tumechukua maoni ya wananchi tangu Mafia mpaka hapa Bagamoyo, wengi wanafikiri kwamba mbunge hastahili kuwa waziri wewe una maoni gani juu ya hilo?” aliuliza Salehe.
Waziri Kawambwa alijibu: “Ni kweli jambo hilo ni tatizo na wananchi wengi wanalifahamu, hususan wa Bagamoyo wanalifahamu zaidi kwani tangu nichaguliwe kuwa mbunge niliteuliwa kuwa waziri. Nadhani  mbunge akiteuliwa kuwa waziri, nafasi yake ya ubunge apewe mtu mwingine au Rais awe huru kuteua waziri nje ya Bunge. Nayazungumza haya kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na ubunge wangu Bagamoyo na waziri katika wizara tofauti.”
Akijibu swali kuhusu ukomo wa kuongoza kwa viongozi wa ngazi za tofauti na urais, Dk Kawambwa alisema ni vizuri nao wakawekewa ukomo na ikibidi iwe miaka mitano.
“Kuna wabunge mle ndani mpaka nawaonea wivu, wamekaa majimboni mwao kwa miaka 35 hadi 40, angalau iwe kwa awamu tatu,  isiwe Rais ana ukomo, lakini wabunge na mawaziri wanaendelea kupokezana vijiti bila ukomo,” alisema Dk Kawambwa.
Kiongozi wa tume hiyo katika Mkoa wa Pwani, Profesa Mwesiga Baregu alipohoji msimamo wa waziri huyo kuhusu ukubwa wa Baraza la Mawaziri baada ya wananchi wengi kutaka lipunguzwe na sambamba na idadi ya wizara.
Akijibu hilo, Dk Kawambwa alisema: “Kwa mawazo yangu binafsi na kwa uzoefu wangu ninashauri suala hilo lisiingizwe kwenye Katiba na aachiwe Rais achague idadi ya watu atakaotaka wamsaidie kutekeleza majukumu yake.”

Wakazi Live in Chicago (@ The Shrine

Vigogo Chadema Kortini kwa kumtusi Mbunge-Mwananchi

VIGOGO wawili wa Chama cha Maendeleo na Demokrasi (Chadema), leo Jumatatu asubuhi wanatarajiwa kuburuzwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapakujibu tuhuma ya kumtolea lugha ya matusi Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Mwigullu.

Vigogo hao ni pamoja naOfisa sera na utafiti wa ChademaMakao makuu,Waitara Mwita Mwikwabe (37) na mshauri wa Chadema na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, DkKitila Mkumbo wotewakazi wa jijini Dar-es-salaam. 

Washitakiwa hao  kwa nyakati tofauti wiki mbili zilizopita,walipandishwa katika mahakama hiyo na kukana kutenda kosa hilo.

Kwa mujiubu wa mwanasheria wa Serikali,Seif Ahmedalidai mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Ruth Massamu kuwa Julai 14, mwaka huu saa 10.00 alasiri huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago wilayani Iramba,washtakiwa bila halali alimtusi Mbunge Mwigullu kuwa ni malaya,mzinzi na mpumbavu huku akijua wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Seif alisema washitakiwa hao bila halali,alitenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali uliolenga viongozi wa Chama hicho kuzungumza na wananchi.

Pamoja na vigogo hao, leo asubuhi vijana nane wakazi wa kijiji cha Nguvumali ya Ndago,Jimbo la Iramba magharibi,wanatarajiwa kupandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa,wakituhumiwa kumw
uuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (CCM) kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Washitakiwa hao ni Manase Daudi (40),Williamu Elia (33),Frank Stanley (20),Charles Leonard (36),Tito Nintwa, Fillipo Edward (30),Paulo Shakilingwa na Emmanuel John Shilla (20).

Mwanasheria wa Serikali mwandamizi, Neema Mwanda,alidai mbele ya hakimu Massamukuwa Julai 14 ,saa kumi alasiri katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago,washitakiwa wote kwa pamoja,bila halali walimpiga kwa kutumia fimbo na mawe  mwenyekiti huyona kusababisha kifo chake.

Vile vile jumla ya washitakiwa 12 wanaotuhumiwa kufanya vurugu katika mkutano huo wa hadhara wa Chadema katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago na kusababisha  kuvunjika kwa amani na utulivu,nao wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mjini hapa.

MNUSO WA KUMPONGEZA BRIGEDIA JENERALI MAGANGA

Brigedia Jenerali Maganga akitoa shukrani zake kwa familia, ndugu jamaa na marafiki kwa kujumuika pamoja katika sherehe ya kumpongeza kwa kukamata Nondoz ya  Diploma In Military Science inayoenda sambamba na Master In Strategic Studies siku ya Jumamosi July 28, 2012 nyumbani kwake, Silver  Spring, Maryland.
Brigedia Jenerali Maganga akipata chakula akiwa na  Waziri mkuu wa moyo wake Love Maganga
keki mbili kweli kukamata Nondoz si  si mchezo
Brigedia Jenerali Maganga akikata keki
Brigedia Jenerali  akipokea zawadi mbalimbali yakiwemo maua aliyoleta kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe. Liliani Munanka (hayupo pichani) , Mercy Dachi (kati) na Mkewe Love Maganga.
Brigedia akiendelea na chakula.
Wageni mbalimbali kutoka kila pembe ya Dunia walikuwepo kwenye sherehe hizo
Mtoto wa Brigedia Jenerali Maganga akiwa amembeba mtoto.
Wageni wakibadilishana mawili matatu.
Wageni waalikwa wkiw na mwenyeji wao.
Kwa picha zaidi Bofya Read More