Baadhi ya wakazi wa jiji wakiangalia pikipiki zilizohifadhiwa nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam jana. Pikipiki hizo zilikamatwa kwa makosa mbalimbali katika msako unaofanywa na jeshi hilo.
-------------------
-------------------
Baadhi ya wapitanjia wakiangalia gari lenye namba T 201 BEQ, lililopata ajali eneo la Ubungo, Dar es Salaam jana. Dereva gari hilo alishindwa kulidhibiti wakati akikimbia baada ya kugonga pikipiki kwenye makutano ya Barabara za Sam Nujoma na Barabara ya Morogoro.
-------------
Mamalishe akimpimia mteja wa chai ambaye alikuwa ndani ya daladala kwenye Kituo cha Shule ya Uhuru Kariakoo, Dar es Salaam jana. Kutokana na ushindani wa biashara hiyo wanalazimika kuwafuata wateja popote.
--------------------
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (HLRC), Bw. Harold Sungusia (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko kwa vyombo vya habari kuhusu vurugu zilizotokea mkoani Mtwara hivi karibuni. Katikati ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Bi. Imelda Urio na Ofisa Usalama Mtandao wa Watetezi Bw. Benedict Ishabakaki.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake