Advertisements

Thursday, April 3, 2014

SIMULIZI TAMU YA WEMA SEPETU


WIKI iliyopita, Wema aliendelea kuelezea simulizi yake tamu ambayo imetokea kupendwa na wasomaji wengi wa Gazeti la Amani. Aliishia pale alipoweka wazi kisa cha kuachana na Chalz Baba, akaeda Marekani, aliporudi akawa na Diamond: Tujikumbushe kidogo kisha tuendelee…

Mwandishi: Nakumbuka ulipoondoka nchini kwenda Marekani ulikuwa na mapenzi na Chaz Baba, lakini uliporejea ikasikika kwamba upo na Diamond, nini kilitokea Wema?
Wema: (kicheko) yeah! Ni kweli kabisa, baada ya kuachana na Jumbe mwaka 2010 kama nilivyosema ndiyo nilianzana na Chaz Baba, nilimpenda, alinipenda. Na yeye ilikuwa tuoane, lakini nimeshasema nikiwa Marekani nilikuwa nasikia leo Chaz alikuwa na huyu, kesho alikuwa na yule, nikamwambia mimi na wewe basi.
Mwandishi: Kwa Chaz Baba mama yako alimkubali awe mumeo?
Wema: Kusema ukweli hakuwa muwazi kwa Chalz Baba, kwamba anamkubali au hamkubali. Lakini ikawa hivyo, tukaachana.
Mwandishi: Baada ya kuachana na Chalz ukajikuta upo kwa Diamond, nini kilikuvutia kwake?
Wema: Nasibu (Diamond) ilitokea kama nilivyokwishasema. Kwa hiyo mtu unajikuta umezama kwake. Wakati mwingine ni vigumu kusema mtu uliyenaye alikuvutia kitu gani!
KUHUSU KIINGEREZA CHA DIAMOND
Mwandishi: Wema, ni kweli Diamond amejua Kiingereza kwa ajili yako?
Wema: Kwanza niweke sawa hapo. Nasibu si kwamba amejua Kiingereza kwa ajili yangu, bali amejua kuzungumza Kiingereza vizuri. Ina maana tangu awali alikuwa anakijua lakini si kivile.
“Mimi na Nasibu tumekaa pamoja mwaka mzima kama mke na mume baada ya mimi kutoka Marekani mwaka ule 2011. Sasa si unajua mimi kidogo nakijua vizuri. Kwa hiyo kwa miezi kadhaa ya nyuma katika kuishi kwetu alikuwa akipata tabu kidogo.
“Ila nataka kukwambia kwamba, Nasibu ni makini sana. Hakuna mtu makini kama yeye. Akiwa hajui kitu lazima akuulize, hakai kimya.”
Mwandishi: Pamoja na sifa zote hizo, lakini mwisho wa siku wewe na Diamond mlimwagana kwa awamu ya kwanza, ilikuwaje?
ALIVYOMFUMANIA JOKATE
Wema: Tuliachana baada ya yeye kunisaliti na Jokate (Mwegelo). Unajua nilimwamini sana na sikuwahi kuwa na shaka naye hata siku moja, nilimwamini kupitiliza nikijua ni wangu na mimi ni wake.
“Lakini nadhani haya mambo ya kumwonesha mtu kwamba unampenda sana ndiyo tatizo. Hasa baadhi ya mwanaume.
“Siku moja nakumbuka nikiwa sina hili wala lile, nikapigiwa simu na rafiki yangu anafanya kazi pale Piccolo, baada salamu akaniambia ‘unajua kama Diamond na Jokate wako hapa na wanapigana mabusu?’
“Nilichanganyikiwa sana, nikachukua teksi, nikaenda.
Kufika, kitu cha kwanza nililiona gari lake likiwa kwenye maegesho. Niliingia ndani, nikawakuta wamewekeana miguu. Niliwasalimia lakini hawakuitika.
“Kwa vile niliona kila kitu niliaga na kuondoka huku nikilia. Usiku Nasibu aliporudi alinikuta napanga nguo kwenye begi niondoke zangu, abaki mwenyewe. Hakutaka kuongea na mimi na mimi sikutaka kuongea naye, tukachuniana. Niliamua kutoondoka lakini mimi na yeye hatukulala kitanda kimoja kwa wiki moja. Alijua naumia lakini hakutaka kuanza.
AMWAGANA NA DIAMOND
“Siku moja isiyokuwa na jina, niliamka nikapanga nguo zangu kwenye begi nikaenda kwa dada yangu, Sinza. Ndiyo ikawa kimoja, nikamwacha yeye aendelee na maisha yake na mimi nikaendelea na maisha yangu. Lakini mimi na Jokate kwa sasa tuko vizuri tu.
Mwandishi: Oke, hiyo ilikuwa awamu ile ya kwanza, si ndiyo?
Wema: Yeah!
VIPI KUHUSU HARTMANN?
Mwandishi: Iliwahi kusemekana kuwa kuna wakati uliangukia kwenye penzi la mjasiriamali anaitwa Hartmann Mbilinyi, ni kweli?
Wema: Yale yalikuwa maneno ya watu. Unajua Hartmann nilikuwa nafanya naye kazi za filamu, wakati ule alikuwa na kampuni yake inaitwa Hartmann Production, watu wakadhani ‘nadate’ naye, si kweli bwana.
BAADA YA DIAMOND, NANI ALIFUATA?
Mwandishi: Wema, unaweza kutuambia mwanaume gani alifuatia baada ya wewe kuachana na Diamond akawa na Jokate?.CREDIT:GPL

Itaendelea wiki ijayo

4 comments:

Anonymous said...

juu ya kuzalilishwa kote bado yuko na diamond kweli unaroho ya paka baby wema sepetu.
yani where is your self esteems as a young lady where is it baby au ndo kuji act bado mdogo.

Anonymous said...

Here we go again, wema please stop giving these people too much info about your personal life, if this was done here in the US diamond had every right to sue you, because what your doing is smear campaign. Mind you he is a man who is single and famous (i mean in africa) so some girls with low self esteem will throw themselves to him. I think your man and possibly husband is sitting somewhere waiting for you. All you have to do is respect yourself (remember respect comes with class). I saw that video from globalp and i must say you behaved badly although i dont want to judge you but honey GROW UP

Anonymous said...

Good advise to you if you want to be a star behave like a star. You said yourself that YOUR CHIZ. Truly your Chiz.

Diamond doesnt deserve all these. Is shame. You need a counselling. YOUR CHIZ.

Unknown said...

Dont blame only diamond hata wewe mwenyewe ulisema yy alikudanganya na ww ukamdanganya na kwa hiyo mumepitia mambo mengi bt nw we lv each other,Galz blame only boyz Y?????