Advertisements

Tuesday, October 14, 2014

ANGALIA PICHA MWANAJESHI ATOA ADHABU KALI KWA RAIA ALIYEVAA NGUO ZA JESHI

Picha unazoona sio utani wala sinema ni raia wa kawaida akiogelea kwenye dimbwi kwa amri ya mwanajeshi.
Raia huyo alikutana na adhabu kali za mwanajeshi huyo baada ya kukutwa amevaa mavazi halisi ya jeshi la Tanzania maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam.
Jamaa huyo alipokamatwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhishaakaamriwa kuvua mavazi hayo na kisha kuaza kutumikia mazoezi ya hatari ..
Haya mavazi raia wanayapenda ila kwenda kutumikia jeshi hawataki ...ahahaaa jamaa alichokipata hawezi kutamani nguo za rangi ya kombat maisha yake yote.

5 comments:

Anonymous said...

Hivi huku si kujichukulia haki mkononi?

Anonymous said...

WANASHINDWA KUTOA HUKUMU NA KUSIMAMIA TA MAANA WANAANGALIA NGUO ZA JESHI. SIWAODE NGUO ZISIZOWEZWA KUIGWA, AMA KWELI ELIMU YA MTU NI ALILI ALOJAALIWA SIO ALOIONGEZEA UJUZI SHULE

Anonymous said...

Yaani ndo faida ya kuwa na wanajeshi wa darasa la saba, Kama amefanya kosa mpeleke kwenye vyombo vya sheria ahukumiwe, sasa hapo ni kuonyesha ubabe na kumdhalilisha raia, safari bado ni ndefu dunia ya tatu yaani bado sana.

Anonymous said...

msiwadharau wa elimu ndogo ya darasa la saba hao walio na ma master na phd D's wamefanya nini au wanafanya nini zaidi ya ufisadi na masifa ya kisomo chao.

walio soma wengi hawako confidence while wasiosoma wapo confidence tena sana,na tunawaona wengi tu kinadharia hawajasoma but maisha yao yako super kuliko hata walio soma.

usimdharau mtu kwa elimu yake sema tu wamekosea hawa polisi kwa vile elimu hawajapata ya kazi zao na mipaka yao.

Anonymous said...

Nafikiri kamuonea huruma sana, kwanini anavaa mavazi ambayo wenzake wameyatolea jasho na kuzamishwa kwenye maji kwa zaidi ya nusu mwaka ili wayastahili...hiyo sio adhabu aliakua anaangalia kama anastahili kuyavaa kwa kumpima ukakamavu, ujasiri na uvumilivu pia.

Safi sana kamanda...akavae ya wafungwa basi