Advertisements

Wednesday, October 22, 2014

CHUO KIKUU ARDHI KUTATUA TATIZO LA UDHIBITI WA MAJI TAKA NA TAKA NGUMU

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na taka ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibaiolojia zinazobadili taka ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibaiolojia zinazobadili taka ngumu au maji taka (waste treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro.Mkemia Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga Akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea kunufaika na teknolojia hiyo ya kibaiolojia ikiwemo kutumika kusafisha maji taka yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa mazingira,wakati wa ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona jinsi teknolojia inavyofanya kazi.Miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibaiolojia zinazobadili taka ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals.

No comments: