Advertisements

Monday, October 13, 2014

WAZIRI LAZARO NYALANDU AZUNGUMZIA TETESI ZA KUTANUA NA AUNT EZEKIEL NCHINI MAREKANI

Baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu(Pichani juu) na msanii wa filamu Aunty Ezekiel kuvinjari nchini Marekani hatimaye waziri huyo 
Aunt Ezekiel
alisema tuhuma hizo zimetengenezwa na kundi la watu ambalo miongoni mwao ni baadhi ya viongozi wa Serikali ambao humchafua kutokana na utendaji kazi wake.

Nyalandu alisema alikwenda Marekani septemba12 kwa ajili ya kufungua tamasha la utamaduni na utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ambako alikutana na msanii huyo mara moja pamoja na mwingine wa Bongo Fleva Kassim Mganga usiku katika moja ya maeneo nchini humo.

Alikana kutanua na msanii huyo kama baadhi ya nyombo vya habari vilivyoripoti na kusema maneno hayo ni kwa lengo la kumwaribia heshima yake mbele ya jamii.

12 comments:

Anonymous said...

Jamani wamuache waziri wa watu, serikali ya bongo ni noma, wapuuzie tu Mr Nyalandu

Anonymous said...

What is kutanua?

Anonymous said...

KWELI WALIKUWA WANATANGAZA UTALII MWAKA HUU TANZANIA ITAPATA WATALII WENGI SANA.
LAKINI KWA NINI ASIMCHUKUWE MKEWE AMBAYA ALIKUWA MISS TANZANIA.

NAWALILISHA MKUU NAOMBA USIIBANE HII COMMENT.

Anonymous said...

Tatizo team ya vijimambo mlifanya makosa kumleta aunt ,alicho kuja kukifanya apa akuna kitu ,ndio matokeo yake mnamtia waziri matatizoni ,inaonekana kama ni kweli lakini kwa watu wengine tunajua niuongo wa magazeti nest time angalia leta mwana mziki ,sio ma movie star atu waitaji ,na kama ni pesa ndio sababu bongo kunawanamziki wengi sana sasa hivi next year my choice is sugua gaga shaha uwe na siku njema mkuu .

Anonymous said...

Jamani muheshimiwa waziri alisema kabisa kwenye hotuba yake kuwa angekuja na mkewe lakini ilibidi aende shuleni kwa watoto kuwakilisha, hata hivyo haituhusu hata kama hakuja na mkewe hayo makubaliano yao kwani viongozi wangapi wanasafiri bila wake zao?? Hiyo sio issue, muacheni waziri wa watu wabongo mnapenda kuongea sana

Anonymous said...

Ilikuwa ni ziara ya kikazi. Haikuwa jukumu lake kumchagua bibie aje naye. Hilo lilikuwa ni juu ya Uamuzi wa vijimambo Blog. Kwa nini wabongo bado wako katika hali ya stone age ya malumbano badala ya kuchapa kazi. Ndio maana bado tuna leg bahind from mind set development which is important to develop the country. Kwa nini wasiandike mambo mazuri ambayo Waziri Nyalandu ameyaleta/ameyabadilisha kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania???

Anonymous said...

Jamani eeh!!baba wa watu aijiheshimu sana,wala hakuwa kama wengi wa viongozi wanaokoromea. Huyo Aunt Ezekiel alitanua na vicheck bob vya hapa mjini saa zote. Mmhkweli nimeamini watz wengine hata hamuogopi Mungu kutunga uongo huu

Anonymous said...

nyinyi magamba wa huko majuu mnamuogopa mungu kwa kumtetea kwa kashfa hii.

Anonymous said...

kutanua is to have good time;somebody how is in holiday vacation,relaxing and enjoying touring around places,eating good and drinking and mixing with ladies/gent etc. That is KUTANUA.

Anonymous said...

serikali ni mimi na wewe na tunawachagua sisi hawa viongozi wanakula kodi la jasho letu sisi walala hoi so tunaona uchungu.serikali kama noma ya bongo wakulaumiwa ni mimi na wewe na kuwakemea kwa vitendo hivi;leo hii eti unasema atupuzi ni kweli atatupuuza na wameshatupuuza kwa kuendeleza kuyafanya haya mambo yao huko kwenu marenaki.

jiulizeni wabeba maboksi nyinyi wa huko marekani katiba iliyopitiswa uraia wenu pachaa mliokuwa mnauomba mmeupata?

si ndo mmepuuzwa huko.watanzania tunasema sana kwa sababu tuna haki ya kusema sana tusiposema sana matokeo yake haya tunapuuzwa tukikaa kimya unadhani itakuwaje.

serikali ya bongo noma kama kwa sababu hatuwakemee wahusikia kwa matendo yao maovu tunawafagilia kwa sababu tunapewa pesa mbuzi za hapa na pale na tunanogewa na kumtetea kama wadau wote humu walivyokuja kumtetea yote wameliswa pesa za kumsafisha na kumtetea.

mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu...

tangazeni utalini wenu lakini mtawajibika tuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

kutanuwa na vicheki bob vya hapa mjini usiku nao pia walikuwepo hao vicheki bob....come on guys;are you for really.

Anonymous said...

yana nakupeni hi 5 comment yangu nilitoa humu ndani mkaituba kwenye takataka na hakuna noma sema ninacho shanga ni kwamba mnazisoma zinakuchomeni miyoo yenu halau mnakuja na kuzijibu humu humu tena na kujifanya kama mdau katuma comment kumbe ni nyinyi wenyewe. aiseeeeeeeeee yesu wangu nyinyi watu mwishooooooooooooooo.

ukilipwa basi ufikiriye wote si wajinga nao kichwani zina chajiii.