Lowassa anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), amesema ana imani kubwa kwamba katika uchaguzi mkuu mwaka huu, hakutakuwa na hila zozote za kuiba kura kwa maslahi ya chama tawala na kwamba wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kumpa ushindi usiokuwa na shaka yeye na wagombea wenzake wote wanaowakilisha Ukawa.
Lowassa alisema hayo jana wakati akizungumza mbele ya umati wa wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa Chadema uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bunju, Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.
Alisema yeye na wenzake wanaounda Ukawa wamejipanga kuhakikisha kuwa hakuna kura inayoibwa.
"Ninachowaomba ni kujitokeza kwa wingi na kutupigia kura kwa nia ya kuleta mabadiliko ya kweli... hakuna kura itakayobiwa," alisema Lowassa na kushangiliwa na umati uliofika kwenye mkutano huo jana.
AJIRA, FOLENI DAR, MAJI
Katika mkutano wake huo, Lowassa alirudia kauli yake kuhusiana na namna anavyoumizwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana na hivyo, akasema mara tu atakapoingia madarakani, miongoni mwa maeneo ambayo serikali yake itayafanyia kazi haraka ni juu ya namna ya kuhakikisha kuwa tatizo hilo linafanyiwa kazi.
Akieleza zaidi, Lowassa alisema njia mojawapo kubwa ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira ni kuzalisha ajira mpya, hasa kwa kuhakikisha kuwa viwanda vingi vinajengwa ili mwishowe viongeze wigo wa ajira kwa Watanzania.
Kadhalika, Lowassa alisema anaguswa na kero ya msongamano wa magari kwenye maeneo ya miji kama Dar es Salaam na hivyo akichaguliwa atahakikisha serikali inamaliza tatizo hilo kwa kuimarisha miundombinu ya barabara, pamoja na kuzipanua zilizopo ili kukidhi mahitaji.
Kuhusiana na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama, Lowassa alisema hakuna njia nyingine ya kuondoa tatizo hilo isipokuwa ni kwa kuhakikisha kwamba serikali inatumia rasilimali zilizopo kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu kwa maisha ya viumbe hai.
Alisema ana uzoefu mkubwa katika masuala ya maji kwani alishaongoza wizara inayoshughulikia maji na hivyo atatumia ujuzi na maarifa yake yote kumaliza tatizo hilo.
MICHANGO YA SHULE MARUFUKU
Katika hatua nyingine, Lowassa alirudia kauli yake ya kuahidi elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.
Alisema ili kufanikisha jambo hilo kwa vitendo, atakapochaguliwa na kuingia Ikulu atapiga marufuku michango yote ya elimu ili kuhakikisha elimu inakuwa bure na hivyo kuwapa fursa Watanzania wote kuipata bila kujali hali zao kiuchumi.
Alisema jambo hilo linawezekana na wala siyo la kufikirika kwani taifa lina rasilimali nyingi ambazo mapato yake yatatumiwa vizuri kuwezesha upatikanaji wa elimu bure kwa kila mmoja.
"Nitafanya kazi kwa spidi 120... jitokezeni na kupiga kura ili tulete mabadiliko ya kweli," alisema Lowassa na kuibua shangwe kubwa.
SUMAYE, MBOWE WANENA
Awali, kabla ya Lowassa kuhutubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bunju na pia kwenye mkutano mwingine alioufanya Mbezi Luis jirani na Stendi ya Mabasi katika Jimbo la Kibamba, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye alisema huu ni wakati mzuri zaidi kwa Watanzania kufanya mabadiliko ya kiuongozi kwa kuking'oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuipa nafasi Ukawa.
Alisema CCM ya sasa haiwezi tena kuleta mabadiliko yatakayowasaidia Watanzania na kwamba hata mgombea urais wao, Dk. John Magufuli, hatakuwa na jipya kwao na hivyo wasifanye makosa siku ya kupiga kura na badala yake wahakikishe wanampa kura nyingi za ndiyo Lowassa na wagombea wengine wa Ukawa.
Kadhalika, Sumaye alijibu mapigo kuhusiana na tuhuma wanazoibuka dhidi ya Lowassa hasa kuhusiana na kashfa ya mitambo ya kufua umeme ya Richmond kwa kuhoji kuwa ni kwa nini Magufuli na timu yake hawaelezi namna watakavyoshughulikia wahusika wa kashfa kama za uchotwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, utoroshaji wa twiga hai na pia ujangili wa meno ya tembo.
"Escrow Lowassa hakuwapo... Magufuli aseme hilo atalishughulikia vipi?
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kujiandaa kupokea mabadiliko kwani CCM haiwezi tena kuongoza nchi.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo ambaye sasa anagombea Jimbo la Kibamba, John Mnyika, alisema ni wakati sasa kwa wananchi wote kuungana katika kumpa ushindi Lowassa na wagombea wote wa Ukawa ili wailetee nchi maendeleo. Aidha, alimtaka Lowassa kuwaondolea kero ya maji wananchi wa Jimbo la Kibamba akiingia madarakani.
CHANZO: NIPASHE
SAWA MZEE KITI HICHO UNACHO,ILA SASA MZEE TULIKUA TUNAOMBA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MPITO BADO SIKU 47 UWAAMBIE TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWAMBA AMANI NA HALI YA BAADAYE YA UTULIVU WA NCHI YETU UPO MIKONONI MWAO.WAWE WAKWELI,WAWAZI,WAMUOGOPE MUNGU. WAPO WATUMISHI WA TUME WENYE UKARIBU NA MAWASILIANO YA HATARI NA VIONGOZI WAKUU WA CCM AKIWEPO PIA DIDAS MASABURI MGOMBEA WA CCM JIMBO LA UBUNGO. WAACHE KABISA NDOTO YA NJAMA ZAO MBAYA.KAMA HAWAONI WAANGALIE YA DR.SLAA AMBAYE YEYE NA MKEWE BAADA YA USALITI WAMEKWISHA IKIMBIA NCHI-HAPAKALIKI-CLOSED CCTV-MPAKA MATUMBONI MWAO.TUNAPOKEA NA KUPATA USHIRIKIANO TOKA KIILA PEMBE YA DOLA NDANI NA NJE YA NCHI.ASANTE RAIA SHUPAVU MWISHO WA SIKU CCM WENYEWE BILA KUSHURUTISHWA WATAKUAMKIA" SHIKAMOO MZEE LOWASSA"
ReplyDeleteNonsensical and wishful thinking!
DeleteAND HENCE YOU ARE A NON- START TANZANAN CITIZEN,REMAIN WHERE YOU ARE.MPO WAJINGA KAMA WEWE ANONYMOUS SEPT 8,2015 at8:31 PM KIBAO NDANI YA CCM NA MLIO NJE YA NCHI KWA FADHILA YA CCM.MWAKA HUU MNAONDOKA MNAKWENDA,HILI NI BARAGUMU LA UMMA UMATI WA WATANZANIA.
ReplyDeleteJAMANI MTOA HOJA WA KWANZA ANONYMOUS SEPT 8,2015 at 8:31 PM AMEWASHAURI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI TANZANIA WAFANYE KAZI ZAO KWA UKWELI WAMWOGOPE MUNGU. WAKATI MTOA HOJA WA PILI ANONYMOUS SEPTEMBER,2015 at 8:31 PM ANAMSEMA MTOA HOJA WA KWANZA MPUUZI.HII MAANA YAKE NINI?MAANA YAKE HUYU NAMBA MBILI HAMUOGOPI MUNGU WAKE ALIYEMUUMBA.NA ALAANIWE VILIVYO HUYU NAMBA MBILI POPOTE PALE ALIPO.LAANA YAKE IUNGANISHWE NA ILE LAANA MAMA YA CHAMA CHA CCM.
ReplyDelete