Advertisements

Monday, November 21, 2016

NDUGU YETU FIDELIS MALOKO ANAOMBA MSAADA WAKO

Ndugu zangu Watanzania wenzangu poleni na majukumu, Mtanzania mwenzetu, ndugu yetu, rafiki yetu na jirani yetu Fidelis Maloko anaeishi Durham, North Carolina anaumwa sana figo zote hazifanyi kazi sasa hivi anatumia mashine, hali yake kusema ukweli ni mbaya na sasa hawezi kufanyakazi tena, pesa yake ya akiba imemalizika kwenye matibabu na dawa.

Huyu Fedelis Maloko ni ndugu yetu, Mtanzania mwenzetu anateseka sana, kama tujuavyo maisha hayatabiriki, mimi na wewe hatujui nini kitatokea kesho na ndugu yetu Fidelis Maloko hakuchagua hali hii aliyokuanayo, ni mipango ya mwenyezi Mungu juu yake.

Naomba kama umeguswa tafadhali msaidie ndugu yetu, mtanzania mwenzako wewe ndiye ngugu yake wa karibu hapa ughaibuni.

Chochote ulichonacho kitabadilisha maisha ya Fidelis Maloko, kwa niaba ya Fidelis Maloko natanguliza shukurani mno kwa mchango wako.

No comments: