Advertisements

Tuesday, December 12, 2017

MRADI MKUBWA WA KUSOMA BILA MWALIMU KWA KUTUMIA TABLETI WAZINDULIWA MUHEZA

Mradi wa majaribio wa miezi 15 wa watoto waliokosa shule, kujifunza wenyewe kwa kutumia teknolojia ya kisasa inayotumia tableti umezinduliwa mkoani Tanga. Mradi huo uliozinduliwa katika kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza ni sehemu ya mradi mkubwa wa miaka mitano wa majaribio duniani chini ya Global Learning Xprize wenye lengo la kutatua matatizo ya kujifunza. Mradi huo hapa nchini unaendeshwa kwa pamoja na Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na XPrize ambao wametoa tableti husika. Aidha kuwezekana kuwapo kwa mradi huo kumetokana pia na makubaliano kati ya serikali ya Tanzania kupitia Wizara yake ya elimu na TAMISEMI na mashirika. Katika utoaji elimu huo watoto wanaohusika ni wa miaka kuanzia 9 hadi 11 na watajifunza kwa kutumia program tano zilizowekwa katika tableti zitakazomuwezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu. Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.[/caption] Mradi huo wa Tanga ambao utagusa watoto 2,400 kutoka katika vijiji 167 vya wilaya za Handeni, Korogwe, Lushoto, Muheza, Mkinga na Pangani unatoa changamoto kwa timu ya wabunifu kuwezesha watoto walio na fursa ndogo ya kuingia katika elimu darasani kujifunza stadi za msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa kutumia tableti wakijifunza wenyewe. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo katika kijiji cha Zenith, Muheza Mkoani Tanga, Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi huo Faith Shayo alisema kwamba mradi huo unaendana na majukumu ya Unesco ya kuhamasisha elimu jumuishi katika kuhakikisha kwamba watoto wote wa Tanzania wakiwemo wa jamii za pembezoni zilizo nyonge zinapata fursa. Alisema UNESCO inatekeleza majukumu yake kwa kuisaidia serikali ya Tanzania kuwezesha kutoa elimu bora kwa wananchi wake wote na hata wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu kutokana na mazingira yao au maeneo yao. Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo akivishwa skafu na kukaribishwa katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kulia ni Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu.[/caption] Alisema Unesco kwa kuangalia mahitaji imekuwa ikisaidia serikali ya Tanzania katika vitu mbalimbali vya kiufundi ili iweze kufanikisha lengo la kuwa na taifa la watu walioelimika hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki katika kazi za kujenga uchumi. “Mradi huu unawapa watoto ambao hawakuwahi kujiunga na shule ya msingi, fursa nyingine” alisema Faith na kuongeza kwamba juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa utaimarisha viwango vya weledi nchini. Faith anasema kwamba kwa sasa japo upo kwenye majaribio utakapofanikiwa utaweza kufanyiwa kazi maeneo mengine ya Tanzania. Aidha Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu alisema kwamba watoto hao wataangaliwa kwa namna ambavyo wanaelewa kila wiki, wanapoenda kuchaji tableti zao.
Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo wakiwasili katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.[/caption] “wakati wa kuchaji pia tunaangalia matumizi ya tableti na ufaulu wa mtoto katika kumaliza porogramu utaonekana na kama ikionekana hasongi mbele itaangaliwa kasoro” alisema Njovu. Alisema kuna vijana 10 wanaojua Tehama na wamefundishwa kusaidia wanafunzi hao katika kuhakikisha kwamba tableti hazikwami au kuharibika. Watu hao wanaoishi vijijini hukohuko pamoja na kulipwa mishahara wamepewa pikipiki mpya aina ya Yamaha kwa lengo la kuhakikisha wanafika kila kata yenye wahusika na kuzungumza nao. Pamoja na tableti hizo pia kumefungwa sola za kuchajia na seva ya kuangalia mwenendo wa watumiaji wa tableti. Kabla ya kuzinduliwa kwa mradi huo watu 282 walifunza namna ya kuhudumia vijana hao ambao wanashiriki katika program. Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, mkoani Tanga, Juma Killo akitoa salamu kwa XPrize, UNESCO, WFP na wageni waalikwa katika hafla hiyo. Wa pili kulia ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo, Afisa Miradi wa UNESCO, Nadia Marques (wa tatu kushoto), Ofisa Elimu wa wilaya ya Pangani, Mbwana Mohamed (wa tatu kulia), Kaimu Ofisa Elimu Lushoto, Beatus Kipfumo (wa pili kulia) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, Xavery Njovu (kulia).[/caption] Katika mafunzo hayo wasimamizi hao ambao wanajulikana kama mama au baba vitongoji walifunza malengo ya mradi na namna ya kuangalia mwenendo wa watoto na mradi wenyewe. Mgeni rasmi katika ukabidhiaji wa tableti, Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu aliwataka wazazi kuhakikisha kwamba tableti hizo zinatumiwa na watoto kwa makusudi yaliyopangwa ili kuwa na taifa la watoto wenye weledi mkubwa. Alisema tableti hizo maalumu ni msaada mkubwa kwa wananchi na serikali hivyo hawana budi kuzitunza na kuzitumia kwa makusudio husika. “teknolojia hii inayowezesha watoto kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu pasipo msaada wa mwalimu ni ubunifu wa kiwango cha juu kabisa” alisema Mayasa na kuongeza kwamba hali hiyo itabadili kabisa fikra za utoaji elimu na kuwakomboa watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu. Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (kushoto) akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza mkoani Tanga, Juma Killo, Mchumi katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Nelson Mwanuna pamoja na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo.[/caption] Aliwataka wazazi kuunga mkono jitihada za serikali kupitia kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa kusaidia kujenga taifa lenye uelewa mkubwa kupitia chanzo cha sasa cha maarifa pasipo msaada wa mwalimu darasani. Alisema msaada huo ni pamoja na kutunza vifaa vyote vya mradi na kutumiwa na wahusika bila kukosa. Aidha alishukuru Shirika la UNESCO, XPRIZE na WFP kwa kuonesha njia na kusema kwamba mkoa utafanya kila linalowezekana kuona mradi huo wa majaribio unafanikiwa. Katika makadihiano hayo watoto zaidi ya 10 walipewa tableti kwa niaba ya wenzao ambao wanashiriki katika mradi. Mmoja wa wazazi wa watoto waliokabidhiwa tableti aliyejitambulisha kwa jina la Musa Ramadhani alisema amefurahishwa sana na mpango huo na kuahidi kuhakikisha kwamba anatunza kifaa hicho ili mtoto wake afaidike nacho. Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo akitoa salamu za UNESCO katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.[/caption] “Mtoto wangu mimi anaitwa Amir Musa na ana miaka 9; hapa tulipo ni ndani sana kupatiwa kifaa hicho kitatusaidia sisi maskini tuliosahaulika kuwa katika utaratibu tena wa weledi” alisema. Aidha alisema kwamba dhamana ya utunzaji inamuangukia yeye kwa kuwa anaamini ni kazi yake kuhakikisha kwamba mtoto wake anapata mafanikio kutokana na mradi huo. Naye mama Kitongoji Hilda Hule alisema kwamba ana uhakika kwamba watoto hao watapata maarifa na kujua kusoma kwa kasi zaidi kwa kuwa hatua za mwanzo zilionesha hamu yao ya kutaka kujua. Anasema kwa upande wake yeye anawaangalia watu wa kitongoji cha Zeneth na anaamini kwamba kwa mradi huo watoto wengi watafunguka. Mmoja wa mateknisheni wa mradi huo ambao watasaidia uwapo wa tableti na program zake Francis Kibaja mwenye makazi yake Korogwe alisema kwamba mfumo huo wa kitabu cha kielektroniki kinamfanya mwanafunzi ajifunze na kujisahihisha na kama watamaliza programu mapema kutokana labda kwa urahisi watawapangia programu ngumu zaidi ili kuwakomaza. Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu akitoa salamu za WFP katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP.[/caption] Aidha alisema kwamba tableti hizo zinagemu kwa ajili ya mtoto akichoka na pia wakati wa mazoezi program itamwambie mtoto kama amekosea au amepatia. Programu zilizowekwa kwa sasa katika tableti hizo ambazo hazina uwezo wa simu ni sawa na mtu kuanza darasa la awali na kuingia shule ya msingi. Katika mradi huo WFP wamepewa dhamana ya kusimamia uendeshaji wa kitengo cha lojistiki na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama-ICT) cha majaribio katika mazingira halisi. Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule ambaye anajukumu la kuchaji na kutunza tableti hizo akitoa maelezo ya namna zinavyotumika kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa watoto wa kijiji hicho.[/caption] Aidha jukumu lake ni pamoja na kuingiza programu katika tableti, kuanzia vituo vya kuwekea umeme unaotokana na jua kwenye tableti hizo vijijini, kusimamia matengenezo, marekebisho na kutoa tableti mpya kipindi chote cha majaribio. Uzinduzi huo ulipambwa na mambo mbalimbali ukiwemo muziki wa asili ambapo kikundi cha JAHAZI ASILI zilitumbuiza kwa ngoma za asili za wakazi wa Tanga na pia muziki wa singeli. Ofisa wa Xprize naye alitumbukia katika burudani za singeli na kuwa burudani kubwa kwa watu ambao walienda naye sambamba na kama yeye alivyokuwa akienda sambamba na wenyeji katika zungusha. Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi programu mbalimbali za kujifunzia zinavyofanya kazi kwenye tableti hizo. Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akisisitiza umuhimu wa wazazi (hawapo pichani) kushiriki katika utunzaji wa tableti hizo kabla ya kuzigawa rasmi. Kushoto ni Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo. Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na mtoto Saidi Hausi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi tableti hizo. Kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa umeme wa sola na Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu na Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo. Mama Kitongoji wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza, Hilda Hule (kulia) akikabidhi tableti kwa mtoto Saidi Hausi huku Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (kushoto) wakishuhudia tukio hilo wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wa pili kulia) akisalimiana na mtoto Juma Saidi wa kijiji cha Zeneth wakati wa zoezi la kukabidhi tableti hizo. Wanaoshuhudia tukio hilo ni kulia ni Mama Kitongoji Hilda Hule mwenye jukumu la kutunza na kuchaji tableti hizo kwa kutumia umeme wa sola, Mwakilishi wa WFP mkoa wa Tanga, ambaye ndiye anayesimamia utekelezaji wa programu hiyo, Xavery Njovu (wa kwanza kushoto), Mwakilishi wa Unesco ambaye pia anasimamia mradi wa Global Learning Xprize, Faith Shayo (wa pili kushoto). Tala Loubieh wa WFP akitoa maelekezo ya jinsi ya kutumia programu ya kujifunza, kuandika kusoma na kuhesabu kwa mtoto Gabu Lakiki mara baada ya kukabidhiwa rasmi tableti hizo kwenye hafla hiyo. Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akiwapongeza baadhi ya watoto wa kijiji cha Zenith ya Kati, wilayani Muheza, mkoani Tanga waliokabidhiwa tableti hizo Baadhi ya wafanyakazi wa WFP wanaotoa msaada wa Tehama kwenye tableti hizo kwa watoto wa kijiji cha Zeneth pamoja wanakijiji wakifurahi jambo katika katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Baadhi wazazi/walezi wa watoto wa kijiji cha Zeneth wilayani Muheza wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Kikundi cha ngoma cha Jahazi Asilia cha wilayani Muheza wakitoa burudani katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Makomandoo wa Skauti wakionyesha umahiri wao wakati wa kusherehesha hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller akijumuika na watoto wa kijiji cha Zeneth kucheza SINGELI wakati wa hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE, Matt Keller aliponogewa na SINGELI katika hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Mgeni rasmi na meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto waliowakilisha wenzao kwenye hafla ya kukabidhi tableti kwa ajili ya mradi wa kutumia teknolojia kujifunza kuandika, kusoma na kuhesabu uliozinduliwa Muheza jana. Mradi huo wa majaribio unafadhiliwa na Global Learning Xprize kwa kupitia UNESCO na WFP. Mkurugenzi Mwandamizi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya XPRIZE ambao ndio wafadhili wakuu, Matt Keller akiwa kwenye picha ya pamoja na Wataalamu wa Tehama walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na vitongoji vyake. Wafanyakazi wa WFP wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa Tehama walioajiriwa na mradi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tableti na mifumo yote ya kusomea zinafanya kazi inavyopaswa katika mkoa wa Tanga na vitongoji vyake.

No comments: