Advertisements

Tuesday, December 12, 2017

TUNAZO RASILIMALI NYINGI LAKINI BADO KUNA HALMASHAURI ZINALALAMIKA HAKUNA MAPATO; DKT NCHIMBI.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mapema leo akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida, kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt Angelina Lutambi.
Naibu Mshauri Mkuu, Maendeleo ya Mfumo wa Mafunzo wa Mpango Shirikishi Jamii kutoka shirika la JICA Naoyuki Shintani akiwa na Mtaalam wa mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo O&OD kutoka OR-TAMISEMI Silas Salamaluku wakijadilia jambo wakati wa mafunzo kwa watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba Linno Mwageni na baadhi ya watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Mwajabu Nyamkomola na Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dkt. Mpamila Madale wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka baadhi ya watendaji wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi amezitaka halmashauri za Mkoa wa Singida kuacha kulalamika kukosa mapato bali watumie vizuri rasilimali nyingi zilizopo, ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuongeza mapato yao.

Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akifungua mafunzo ya kutambua fursa na vikwazo kwa ajili ya kupanga miradi ya maendelo kwa jamii (O&OD) yaliyoandaliwa na ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa watendaji wa halmashauri zote za mkoa wa Singida.

Amesema Mkoa una fursa nyingi katika sekta ya kilimo, utalii, ufugaji, madini na uvuvi ambazo bado hazijatumiwa vizuri na halmashauri katika kukuza uchumi wa viwanda kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wa Singida.

“Singida ina zalisha Vitunguu vingi na bora nchini, ina zalisha viazi zitani vingi na vyenye ubora, singida pia ni mzalishaji mkubwa wa alizeti na mafuta ya alizeti huku tukiwa na viwanda zaidi a 120 vya kusindika mafuta ya alizeti, katika sekta ya utalii tuna vivuti vngi ikiwemo bwawa la kuongelea ‘swimming pool’ lililojengwa na mjerumani na lipo katikati ya pori lakini vyote hivi hatujavitumia vizuri,” amesisitiza Dkt Nchimbi.

Dkt Nchimbi ameongeza kuwa halmashauri zinapaswa kutotumia mafunzo hayo kulalamika bali mafunzo hayo yawajengee uwezo wa kutambua wapi kuna pengo katika maendeleo ya jamii na kisha kuanisha fursa na mikakati ya kuzitumia fursa hizo kuziba pengo hilo.

Aidha amewataka kutumia fursa ya malengo na mitazamo waliyonayo ambayo inaweza kuleta maendeleo pamoja na kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanawajengea uwezo wa kubaini na kuitumia ajenda ya fursa na vikwazo katika maendeleo kwa ngazi zote.

Dkt Nchimbi amesema matarajio yake ni kuona kila mshiriki wa mafunzo hayo ana mabadiliko ya tabia katika utendaji wake ambapo mabadiliko hayo yanaweza kupimika aidha kwa macho au viashiria vingine.

Ameongeza kuwa matarajio ya mengine ni kuwa na Singida mpya yenye takwimu sahihi za bidhaa zote zinazozalishwa Mkoani Singida ili kuzitumia takwimu hizo katika kupanga mikakati ya maendeleo pamoja na kutangaza fursa zote zilizopo Mkoani hapa.

Dkt Nchimbi ameeleza kuwa mafunzo hayo wamepatiwa ili kutatua changamoto zilizopo na endapo kutaendelea kuwepo kwa changamoto hizo katika sekta mbalimbali ikiwemo za kilimo, afya, maji, elimu, barabara na utawala bora basi tumi nzima ya fursa na vikwazo itakuwa imeshindwa.

No comments: