Advertisements

Thursday, May 23, 2019

NEC yawataka wasimamizi wa uchaguzi kuzingatia katiba na sheria kusimamia uchaguzi mdogo kata 32

 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akizungumza wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
 Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wakila kiapo mbele ya Hakimu Arnold Kirekiano wakati wa kifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R ) Mbarouk Salum Mbarouk (wa pili kushoto) akiwa na Wajumbe wa Tume Jaji (Mst.) Mary Longway na Mhe. Asina Omari (kulia) wakiwa an Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia (kushoto) wakifuatilia mada. Picha na NEC 

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mbarouk Salum Mbarouk amewataka  wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria zinazosimamia uchaguzi nchini katika kusimamia uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 32 unaotarajiwa kufanyika Juni 15 mwaka huu.

Jaji Mbarouk ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi kwa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka kata 32 na halmashauri 20 za Tanzania Bara zinazotarajia kushiriki katika uchaguzi huo, yanayofanyika jijini Dodoma.
Alisema pamoja na baadhi ya wasimamizi kuwa na uzoefu katika kusimamia chaguzi mbalimbali, aliwasisitiza kuzingatia maelekezo watakayopewa na Tume katika kusimamia uchaguzi huo badala ya kusimamia kwa mazoea kwani NEC imewaamini kuwa wanaweza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria.

“Ndugu washiriki mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na kuteuliwa kwa sababu mnao uwezo wa kufanya kazi hii jambo la muhimu ni kujiamini na kujitambua na kwamba mtapaswa kuzingatia sheria, miongozo, kanuni na maelekezo yanayotolewa na Tume kwa ajili ya kuendesha na kusimamia chaguzi” alisema Jaji Mbarouk.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Athumani Kihamia aliwataka wasimamizi hao wa uchaguzi kuwepo muda wote wakati wa kutekeleza majukumu ya uchaguzi na hata pale inapotokea dharura wahakikishe anakuwepo msimamizi atakayetekeza majukumu yao.
“Ni vyema mkafahamu kwamba kipindi hiki ambacho mmeshateuliwa na kuapa kuwa wasimamizi wa uchaguzi, wewe unakuwa mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa muda huo.Kwa hiyo ni vyema ukawa ofisini muda wote ukiondoa dharura” alisema Dkt. Kihamia.

Alifafanua kuwa suala hilo limetolewa muongozo katika Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 sehemu ya 4 (1), watendaji wote wa uchaguzi katika kipindi cha uteuzi wa wagombea, katika kipindi cha upigaji kura na katika hatua yoyote ya mchakato wa uchaguzi.
Katika mafunzo hayo, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walikula kiapo cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa mbele ya Hakimu Arnold Kirekiano ambapo mada mbalimbali zitawasilishwa kuhusu hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.

No comments: