Advertisements

Sunday, March 29, 2020

Aliyetoweka nyumbani, mwili wake wakutwa hauna kichwa, miguu na mikono

By Daniel Makaka, Mwananchi mwananchipepars@mwananchi.co.tz

Sengerema. Sarah Nestory (20) mkazi wa kitongoji cha mission wilayani Sengerema Mkoa Mwanza nchini Tanzania aliyetoweka nyumbani siku saba zilizopita, mwili wake umekutwa kichakani umeharibika vibaya.

Nestory Costantine ambaye ni baba mzazi wa Sarah amesema mwanaye alitoka nyumbani Machi 23,2020 asubuhi kwenda shambani kupanda karanga lakini hakurejea hadi jana Ijumaa mwili wake ulipokutwa kichakani.

Amesema walimtafuta maeneo mbalimbali bila mafanikio hadi jana Ijumaa kumwona mtu akiponda kokote kwenye mlima mbali na nyumbani kwako kumuuliza kama amemwona binti yake, “na yule akasema ameona ndani ya ule mlima kuna inzi wametapakaa.”

Costantine amesema walikwenda eneo hilo na kukuta mabati ya mwili wa binti yake, “kwani kichwa, mikono na miguu haipo yote.”

Amesema kilichowafanya wamtambue ni nguo alizokuwa amevaa siku anatoweka nyumbani zilikuwa kando ya mwili wa binti huyo, mbegu za karanga na simu ya mama yake aliyokuwa ameondoka nayo kwenda shambani.

Amesema walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua mwili wa Sarah na kuupeleka hospitali kwa uchunguzi kisha leo Jumamosi Machi 28,2020 wameurejesha kijijini Mission kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika baadaye.

Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha kutoka kwa tukio hilo kusema wanaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika na mauaji ya binti huyo aliyehitimu kidato cha nne mwaka 2019 Shule ya Sekondari Ngeli.

No comments: