Advertisements

Wednesday, September 23, 2020

ZAIDI YA WANAWAKE 1,700 MKOANI IRINGA WAJITOSA KUTAFUTA KURA ZA DR JOHN POMBE MAGUFULI

Mgeni rasmi ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Telesia Mtewele akiongea na wanawake waliojitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM
Baadhi ya wanawake waliokuwa wamejitokeza kwenye kongamano hilo la kimkakati la kutafuta kura za wagombea wa CCM

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Zaidi ya wanawake 1,700 mkoani Iringa wamejipanga kuhakikisha wanazitafuta kura za mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli ili aweze kuwa Rais wa Tanzania.

Akizungumza kwenye kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi(CCM) Telesia Mtewele alisema wanawake wa mkoa wa Iringa wanapaswa kuyaeleza mambo ambayo Rais Magufuli amefanya kwa kipindi cha miaka mitano.

Alisema kuwa Rais Dr Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na amefuta michango shuleni hivyo wanawake wa Iringa wanapaswa kumtafutia kura Dr John pombe Magufuli.

Mtewele aliongezea kwa kusema kuwa katika sekta ya elimu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wanapana mikopo kwa wakati na ndio maana kwa kipindi cha miaka mitano hakuna maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma.

Alisema kuwa Rais Dr John pombe Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya afya kuwa kujenga vituo vya afya zaidi ya 400,hospitali za wilaya,kuongeza bajeti ya dawa kwenye hospitali zote,kuajili wafanyakazi wa sekta ya afya na ameboresha huduma za upasuaji kwenye hospitali zote za rufaa hivyo wanawake wanajifungua bila shida kama ilikuwa hapo awali.

Mtelewe aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa kutumia ushawishi wao kuhakikisha wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dr John pombe Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea wengine.

Aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa kwenda kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia udiwani,ubunge hadi urais hivyo wanawake waliohudhulia kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuhakikisha CCM inapata kura za kutosha kuliko vyama vingine.

Kauli mbiu yetu ni wanawake wa Iringa tunakwenda na Magufuli na ndio lengo la kongamano hilo ni kuhakikisha tunatafuta kura za kutosha kuliko vyama vingine vyote na kuendelea kushika dola kama ilivyokuwa kawaida ya chama cha mapinduzi (CCM).

Naye mratibu wa kongamano hilo Dr Ritta Kabati alisema kuwa mgombea wa urais wa chama cha mapinduzi Dr John pombe Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika nchi hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa wameamua kumuunga mkono mgombea huyo.

Alisema kuwa zaidi ya wanawake 1,700 walijitokeza kwenye kongamano hilo ambao lilifikia lengo la kuhakikisha wanawake wa mkoa wa Iringa wanazitafuta kura za chama cha mapinduzi kwa njia yoyote ile ili kuwapa ushindi wagombea wa CCM.

"Kongamano hilo liliwakutanisha wanawake kutoka kwenye sekta mbalimbali kama vile wafanyabisha,wanawake wanaouza kwenye bar,grocery,vilabuni,dini,taasisi mbalkabati,walemavu,machinga,wakulima,walimu,madaktari n.k hivyo kongamano hilo lilifanikiwa kugusa sekta zote"alisema Dr kabati

Dr kabati aliwaomba wanawake wa mkoa wa Iringa waendeleee kuwaelimisha wananchi wengi ambao wanapiga maendeleo yalifanywa na Rais Dr John pombe Magufuli ili waweze kumpigia kura nyingi mgombea huyo ashinde kwa kishindo

Aidha Dr kabati alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano aliyokuwa Rais amefanikiwa kuboresha sekta zote kwa kiasi kikubwa hivyo wanawake wa mkoa wa Iringa wanapaswa kuzitafuta kura nyingi za mgombea huyo wa CCM.

kwa upande wake mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu alisema mwanamke ni nguzo kubwa katika amani ya jamii kwa kuwa mara zote amekuwa akijishusha katika mambo mbalimbali na hivyo kuleta amani.

Msambatavangu amesema wanawake wa Iringa wanakila sababu ya kuwachagua viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu katika kipindi cha miaka 5 iliyopita kimewahudumia vizuri na pia kimeonesha kutaka kuwahudumia vizuri kutokana na ilani ya chama hicho ya mwaka 2020.

No comments: