Advertisements

Friday, January 27, 2023

YANGA NA SIMBA UGHAIBUNI KUNOGESHA OLD SCHOOL REUNION JUNE 17, 2023 DMV

Timu ya Yanga Ughaibuni
Timu ya Simba Ughaibuni


Na Mwandishi wako, Washington, DC
Mtanange wa Yanga na Simba Ughaibuni utafanyika Jumamosi ya June 17, 2023 DMV, timu hizi zinazoundwa na mashabiki wa timu hizi na baadhi ya wachezaji waliochezea timu hizi zamani hua na msisimuko wa pekee na yote ni katika kunogesha bash kubwa la aina yake la Old School Reunion ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.


Tamsaha hili la Old School Reunion halikufanyika kwa miaka 2 mfululizo kutokana na Dunia kukumbwa na janga la Uviko-19, mara ya mwisho tamasha hilo kufanyika ilikua mwa 2019 Houston, Texas na Yanga ikiambulia kichapo.


Old School Reunion hukutanisha vijana wa zamani kutoka kila pembe ya Dunia na kukumbuka enzi zile walizokua wakiruka nyoka na burudani hii uletwa kwenu na madj mahili wa old school nchini Marekani, Dj Luke Joe akishirikiana kwa karibu na Dj Dennis (ThaFunkHouse) katika kuhakikisha moja na mbili haiendi kombo.


Old School Reunion ya mwaka huu itarajiwa kuwa ya aina yake kutokana kwamba haijawahi kutokea ndani ya miaka miwili na pia kuna uwezekano wa kupata wageni mashuhuri kutoka Tanzania kwa sasa ni mapema sana kutaja majina yao lakini kadri muda utakavyokaribia majina yao yatajulikana.


Old School Reunion inatarajiwa kufanyika katika ukumbi waWest Bowie Village Hall mara tu baada yaa mtanange wa Yanga na Simba, taarifa zaidi zitafuata, karibuni sana katika jiji la watunga sheria.

No comments: