Monday, June 24, 2024

NAIBU WAZIRI KHAMIS AHIMIZA WANAFUNZI KUTUNZA MAZINGIRA



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akikaribishwa kwa ajili ya kuongoza Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akihutubia wakati wa Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akishiriki zoezi la upandaji wa miti alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024.


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akikabidhi vyeti kwa wahitimu kwenye Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024.



Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanafunzi wakati wa Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimiza wanafunzi na wananchi wote kwa ujumla kuona umuhimu na kulipa uzito suala la usafi wa mazingira kwa ustawi wa nchi.

Ametoa wito kwa taasisi za kifedha, mashirika mbalimabali na vyuo kuendelea kushiriki katika kampeni za usafi mazingira safi na kuwasaidia wanafunzi wenye tunu ya kushiriki kikamilifu.

Mhe. Khamis ametoa wito huo kwenye Mahafali ya Tatu ya Klabu ya Mazingira ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Juni 22, 2024 na kusema Serikali itaendelea kusimamia usafi kuhakikisha taifa linapiga hatua katika utunzaji wa mazingira.

Amesema ni muhimu kuendelea kutolewa kwa elimu ya mazingira hasa katika vyuo hatua itakayosaidia kuchagiza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na kutokulindwa ipasavyo kwa mazingira katika nyanja mbalimbali za maisha.

Halikadhalika, Naibu Waziri Khamis amesema ujumbe wa mwaka huu wa mahafali hayo "Tunza Mazingira na Wewe Yakutunze" unahimiza kuwa suala la usafi wa mazingira ni jambo nyeti kwa afya, ustawi na maendeleo ya kila mtu.

“Kupitia mahafali haya nawasihi wanafunzi kuendelea kuwa mfano bora wa kuendeleza harakati za kulinda, kutunza na kudumisha mazingira katika maisha ya kila siku kuonesha taaswira kwamba taaluma zao sio ombwe tupu bali zimebeba mategemeo na uelekeo ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile Mapinduzi ya Zanzibar,” amesema.

Aidha, Mhe. Khamis amewapongeza wanafunzi hao kwa kuonesha wazi ukomavu wa fikra yakinifu kwao na walimu wao kwa elimu ya utunzaji wa mazingira chuoni na hivyo kuamsha hamasa ya kushiriki kwa vitendo zoezi hilo pamoja na changamoto wanazopitia.

Mahafali ya Klabu ya Mazingira ya SUZA hufanyika kila mwaka kwa kila wanafunzi wanaomaliza masomo yao kwa ngazi mbalimbali ili kutathmini maendeleo ya utunzaji wa mazingira chuoni, kuhamasisha utunzaji na ulinzi wa mazingira.

No comments: