tag:blogger.com,1999:blog-6324088563257897474.post4256142624957441134..comments2024-02-26T05:08:35.775-05:00Comments on VIJIMAMBO: BILIONEA SABODO AKITOSA CHADEMA AAHIDI KUTOA TRILIONI 10 ZA KUWEKEZA DODOMA ILI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULIVIJIMAMBOhttp://www.blogger.com/profile/09023266887599892472noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-6324088563257897474.post-2759531803129815272016-08-03T01:04:26.930-04:002016-08-03T01:04:26.930-04:00Safi sana kizuri kitajiuza tu hata kama watu wataj...Safi sana kizuri kitajiuza tu hata kama watu watajaribu kukitia dosari na kibaya hata kama kitapakwa rangi nzuri na kutembeza hapa na pale lakini mwisho wa siku kitaishia kudoda tu. Licha ya kelele na unafiki wa upinzani juu ya Magufuli kuna nguvu moja tu ambayo mwisho wa siku ndio itakayotoa jawabu kati ya haki na batili na nguvu hiyo sio nyengine bali ni nguvu na jicho la M/Mungu alietukuka. Maghufuli ni mtanzania mwenzangu amapo imetokana kuwa na imani tofauti za dini kama ilivyo kwa watanzania utafauti wetu wa dini au kabila si kitu kinachotuondeshea mshikamano wetu na Mungu azidi kutupa baraka juu ya hili Amini. Lakini kubwa kuliko yote ni Ukweli na uadilifu wa hali ya juu katika utendaji wake wa kazi wa Magufuli,jambo ambalo linanifanya kumsapoti muheshimiwa Maghufuli na nitaendelea kumsapoti labda nijiridhishe yakuwa anafanya mambo ya hovyo ya kutengua uadilifu wake aliokuwa nao sasa na sio yale makosa ya kibinaadamu kwani Magufuli ni binadamu pia kukosea ni lazima. Tunaimani kabisa yakwamba kama mueshimiwa Magufuli na serikali yake wataendelea na kasi hii hii ya nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi basi kuna akina Muheshimiwa Sabodo wengi tu kutoka nje na ndani ya Tanzania watakaokuja kuekeza. Inashangaza sana unapoona wapinzani wakimpiga vita Magufuli kwa nia yake nzuri ya kupambana na kuhakikisha maisha ya mtanzania yanakuwa bora. Kwa kiasi fulani ni jambo la kusikitisha na kwa bahati mbaya inaokena hata baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vinashiriki katika kuupotosha umma juu ya kazi nzuri na ngumu anayoendelea kuifanya Magufuli. Mueshimiwa raisi anahitaji kuungwa mkono na watanzania wote wenye kuitakia mema Tanzania kwa nguvu zetu zote. Wale waliokuwepo kule nyumbani,wa Europe,wa Amerika, wa Asia, wa America kusini,Australia nakadhalika nakadhalika bila ya kujali tofauti zetu za kisiasa kwani kiuhalisia hatumsapoti Magufuli bali tunaisapoti Tanzania yetu. Kama wewe ni mpinzani na unahasira au wivu na kasi ya Maghufuli sidhani kama busara kupika majungu na kupita kusambaza uongo, badala yake kama unaweza zidisha kasi yako ya maendeleo izidi ya Magufuli jitahada zako zitaonekana kama anavyoonekanwa Magufuli hivi sasa. La kama mpinzani huwezi kuizidi kasi yake basi muunge mkono na kama huwezi kumuunga mkono basi ni bora kukaa kimya kuliko kumpiga vita na kumvunja moyo kwani mwisho ya siku watu makini na wenye uchungu na nchi waliokuwa wanasapoti wapinzani kwa manufaa ya Tanzania kama akina Muheshimiwa Sabodo watawacha mkono mmoja baada ya mwengine ni jambo la hatari kuwa na upinzani dhaifu nchini bado tunahitaji upizani imara wa kuipa CCM changamoto lakini kwa upinzani huu tuliokuwa nao unaongozwa na akina Mbowe wakupinga kila kitu anachofanya Magufuli hata vile vitu ambavyo havihitaji hata kuambiwa kuwa ni jambo nzuri kama vile kupigania watoto wote wa kitanzania wanapata Elimu ya lazima na bure basi kwa upinzani kushindwa kutambua angalau hilo kwa hakika hakuna faida ya upizani tuliokuwanao wa kisiasa Tanzania kwani si upizani bali ni fitna. Hata kama kutakuwa na mapungufu kwa yale alioyaanzisha muheshimiwa Maghufuli kiukweli ni kwamba kitu chochote kinahitaji maboresho na hapo ndipo watanzania utilitarajia upizani kuonesha uwezo wao jinsi gani wangetoa mchango wao juu ya maboresho ya yale aliyaanzisha Magufuli lakini badala yake tunashuhudia dharau na kejeli kwa kweli inasikitisha,upizani mmetuangusha hiyo sio aina ya demokrasia tulioitarajia kutoka kwenu. Ningechukua nafasi kumpongeza muheshimiwa Sabodo kwani yeye ni mtanzania na mzalendo wa kweli.Anonymousnoreply@blogger.com