Advertisements

Friday, June 10, 2011

Marekani yapongeza Polisi kumkamata Mama Leila

Na Godfrey Ismaely

UBALOZI wa Marekani Nchini umeipongeza serikali pamoja na Jeshi Polisi kwa jitihada zake za kufanikiwa kumtia mbaroni mwanamke Raia wa Kenya 
anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Bi. Naima Mohamed Nyakiniwa "maarufu Mama Leila), ambaye alifikishwa mahakamani hivi karibuni.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka ubalozi huo, jitihada hizo za Jeshi la Polisi za kumkamata mwana mama huyo na wenzake watatu,  zimeonesha uwajibikaji mzuri.

"Marekani kupitia ubalozi wake hapa nchini inapenda kuipongeza serikali hasa Jeshi la Polisi kwa kufanikisha zoezi muhimu Juni Mosi, mwaka huu ambalo liliwezesha kumkamata Mama Lela na wenzake watatu," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa zaidi ya kilo tano za dawa ya kulevya zilipatikana zimefichwa eneo ambalo Mama Leila alikuwa amekaa.

"Mama Lela alikamatwa kufanikisha notisi ambayo ilitolewa kwa Taasisi ya Polisi wa Kimataifa (ITERPOL) mara baada ya Ujerumani kuridhia kutoa kibali ili akamatwe kutokana na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa muda mrefu," imefafanua sehemu ya taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na kuongeza

Taarifa hiyo inamtaja Mama Leila kuwa amekuwa akijihusisha na biashara ya dawa hizo katika Nchi za Afrika ya Mashariki kwa miaka mingi na kuwa Ikulu ya Marekani ilimtambua na wenzake sita kwa kuwa na mitandao mipana ya kuuza unga katika ngazi za Kimataifa, hivyo kupitia sheria mpya ya kudhibiti dawa hizo na hata kuwataja wahusika hiyo ni hatua nzuri.

"Nchi ya Marekani ilifanya hivyo kupitia sheria hii inayotoa nguvu ya kuwataja wahusika na hata kuwachukulia hatua pamoja na taasisi zao zinazowapatia udhamini sehemu yoyote hapa duniani," iliendelea kufafanua taarifa hiyo na kuongeza.

"Pia wahusika wa madawa ya dawa hizo licha ya kuchukuliwa hatua kali za kisheria, biashara zao zinafilisiwa na raia wa Marekani, wakichukuliwa hatua zaidi pamoja na mali zao kuzuiwa popote," iliongeza taarifa hiyo.


CHANZO:MAJIRA

No comments: