Advertisements

Saturday, May 18, 2013

MBUNGE AANGUKA BUNGENI LEO

MBUNGE wa Viti Maalum, pichani Mwanamrisho Taratibu Abama (Chadema), ameanguka bungeni, baada ya kujisikia vibaya.

Mbunge huyo alianza kujisikia vibaya, hali iliyomfanya kuketi katika viti vilivyo karibu na zahanati ya Bunge.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia walisema mbunge huyo alipata huduma ya kwanza katika zahanati hiyo kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Dodoma.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya hospitali hiyo, zinasema mbunge huyo alilazwa wodi namba 18.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dk. Zainab Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mbunge huyo.

“Ni kweli yupo hapa na hali yake inaendelea vizuri sasa ,”alisema.

2 comments:

Anonymous said...

Nafikiri alikuwa hajapata breakfast

Anonymous said...

wacha utani wewe mdau wa mwanzo wabunge wana kula na kunono hivi wasipate break fast nafikiri kwa vile bongo watu hawa fanyi physical check ups kwa mwaka so huwezi kujua labda ana blood pressure au kisukari etc mambo mengi tu binadamu yanamkumba mpaka unaanguka si yo eti break fast

na linginewe labda wamemuangia, wachawi wako wengi bongo huko hakuendeki ukitaka ukuu lazima ujigange na kujigangua kazi kweli bongo