Baraza la madiwani wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni limepitisha bajeti ya sh.bilioni 121 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya halmashauri kwa mwaka
wa fedha wa 2014/2015.
Akitoa taarifa hiyo Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Yusuph Mwenda alisema fedha hizo
zimetokana na makusanyo ya vyanzo vya mapato , pesa kutoka ruzuku
serikali kuu,Tamisemi,pesa za makusanyo ya ndani ya Halmashauri .
Kwa sasa Halmashauri ina uwezo wa
kujiendesha kwa asilimia 30 tofauti na hapo nyuma ambapo ilikuwa
ikijiendesha kwa asilimia 20 tu.
Bajeti ya mwaka 2014/2015 ina lengo
la kutekeleza mipango ya maendeleo na kuwaondolea umaskini wakazi wa
kinondoni na kuboresha maisha yao.Imetolewa na Manispaa ya Kinondoni.
CHANZO: MTAA KWA MTAA
No comments:
Post a Comment