Advertisements

Tuesday, May 13, 2014

JINSI YA KUMSINGA (massage) na KUMSUGUA (scrub) MWENZA WAKO KWA KUTUMIA VITU ASILIA.

Binadamu wote lazima tuchoke wakati fulani na kupata maumivu ya viungo vya miili yetu.Basi si kila siku tuwe tunakimbizana kwenye massage lounge,siku moja moja unatakiwa umsugue na kumchua mwenzio nyumba.
Oga vizuri kabla ya kuanza shughuli hii, inaweza fanywa kitandani au kwenye mkeka. Unaanza kuusugua mwili wote kwanza kwa kutumia unga wa liwa na unga wa karafuu ulichanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi au unga wa manjano uliochanganywa na maji ya rose pamoja na machicha ya nazi. Sugua mwili mpaka uhisi uchafu na nongo zote zimeisha.Baada ya hapo unaoga nakurudi kwa ajili ya kusingwa.Unachukua mafuta ya mzaituni,ya nazi au ya ufuta unampaka mwili mzima na kuanza kumsinga(kummassage) taratibu na kwa upendo alafu unachukua unga wa karafuu na kuunyunyuzia mwilini sana sana sehem za mgongoni na kiunoni(unga huu usiguse sehem za siri,unawasha).Utaendelea kumsinga mpaka utakaporidhika unamuacha akae na ule unga kama dakika 15 hivi,akipitiwa na usingizi muache apumzike akiwa macho akaoge au ukamuogeshe alafu kitakacho fuata  hatutaki kujua..........
Kusugua na kusinga mwili inasaidia kuondoa uchafu mwilini,kupunguza maumivu makali mwilini,inakufanya upate pumziko na kuondoa usongo wa mawazo , kutaiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu katika mwili wako.Pia huleta furaha kwa wale wawili wapendanao.

No comments: