Advertisements

Friday, April 7, 2017

DC KASESELA AWATAKA WANANCHI KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo

Na Fredy Mgunda,Iringa

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wananchi wa wilaya ya iringa kuacha tabia ya kuamini na kujihusisha na maswala ya imani za kishikina pamoja na kujichukulia hatua mikononi.

Ameyasema hayo baada ya kuwepo kwa taarifa za mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mikong’wi kata ya kihologota wilaya ya iringa ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa kichwa na kutelekeza kiliwili chake.

“Kwanini watu wajichukulie hatua mkononi wakati serikali,jeshi la polisi,mahakama,makanisa na misikiti huku ndio unaweza kutatuliwa shida zako zote  na haya mambo ya kishikina serikali haiamini da nasikitika sana kwa tukio la leo ni baya sana”alisema Kasesela

Kasesela alisema kama wilaya wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kuwataka wananchi wote kutojichukulia sheria mikononi kwa kuwa serikali haiamini uchawi na kwamba ameliagiza jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini aliyehusika na tukio hilo.

“Wilaya ya Iringa ilikuwa imetulia sasa yameanza mambo ya kuuwana kwa keli lazima jeshi la polisi lifanye uchunguzi kwa kina kubaini nini kinachoendelea katika kijiji cha mikong’wi na lazima tukomeshe na kuwa elimu wananchi kutojihusisha na maswala ya kishirikina kwa kuwa serikali haiamini sala hilo”alisema Kasesela 

Kasesela ameeleza kuwa tukio hilo limetokea asubuhi ya leo na kumtaja aliyefariki dunia kuwa ni hasani nyalusi mkazi wa kijiji cha mikong’wi tarafa ya Isman mkoani Iringa.

Aidha Kasesela amewaomba viongozi wa dili mbalimbali kutoa elimu ya mungu na kukemea maswala ya kishikina kwa kuwa yanapunguza nguvu kazi za wananchi.

<!--[if gte mso 9]>

No comments: