Advertisements

Friday, April 21, 2017

HALIMASHAURI YA MBARALI YATAKIWA KUWEKA MIFUGO YOTE CHAPA ILI KURAHISISHA UDHIBITI WAKE KATIKA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi akiongea na Waandishi wa habari wakati wa mkutano na Wananchi (hawapo pichani) wa kata ya Madibira Wilayani Mbalari.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

Halimashauri ya Wilaya ya Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng'ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa chapa ili kurahisisha kuweza kujua ng'ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia kila mfugaji awe na ng'ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia uharibifu wa mazingira uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi. Katika maagizo hayo pia Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa kushirikiana na Wananchi wake kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na kuingizwa kwa mifugo katika mto Ndembela kwa ajili ya kunywa maji.

Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea na Wananchi wa kata ya Madibira wakati wa mkutano na Wananchi juu ya kujua na kufahamu changamoto mbalimbali zinazosababaisha uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito inayozunguka Mto wa Ruaha Mkuu ukiwemo mto Ndembela.

Akiongea katika Mkutano huo Bwana Muyungi pia ameahaidi kushughulikia Wawekezaji ambao siyo waaminifu wanaotumia maji bila kibali cha Serikali au wale ambao wanazidisha kiwango cha uchukuaji maji tofauti na kile kilichoanishwa katika kibali . Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu na kuhakikisha rasilimali zote zilizopo Nchini zinatumika kwa usahihi .

Akijibu hoja hizo Mhe. Diwani wa Kata ya Madibira kwa niaba ya Mkurugenzi aliahidi Halimashauri hiyo kuyafanyia kazi mambo yote waliyoagizwa kuyafanya. Aliongeza kuwa atasimamia yote na pia atashirikiana na Wananchi wa Madibira kuhakikisha maagizo yote yanapatiwa ufumbuzi.

Baada ya Mkutano huo pia Wajumbe wa Kikosi kazi hiko walipata fursa ya kutembelea shamba la mpunga la chama cha Wanaushirika Madibira (MAMCOS) kwenda kujionea shughuli mbalimbali za utunzaji wa maji kwa ajili ya kilimo zinavyofanyika. Akiongea baada ya kutembelea shamba hilo la hekta 3000, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja aliwapa agizo la kuweka geji itakayodhibiti kiasi cha maji yanayotoka shambani baada ya matumizi ya umwagiliaji kufanyika. Pia wametakiwa kutengeneza miundo mbinu shambani ili kuwezesha barabara ya shambani hapo kupitika kwa urahisi na maji kutomwagika hovyo. Pia kusafisha shamba lao mara moja kuondoa nyasi na magugu yalioota kwenye mifereji ya kupitishia maji shambani hapo.Kikosi hiko cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kiliundwa na Makamu wa Rais wa Tanzania kikijumuisha Wajumbe kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kikosi kazi hiko kimegawanyika katika makundi matatu (Iringa, Mbeya na Njombe.

No comments: