Advertisements

Sunday, April 16, 2017

MAMIA YA ABIRIA WAKWAMA NJIANI BAADA YA LORI LILILOBEBA MAKAA YA MAWE KUPATA AJALI NAMTUMBO MKOANI RUVUMA.

Watu watatu wamenusurika kufa huku mamia ya abiria wanaosafri kuelekea Dar es Salaam  na mikoa ya Lindi na  Mtwara na wanaotokea mkoa wa Ruvuma wakielekea  mikoa hiyo wakikwama njiani  baada ya roli lililobeba makaa ya mawe aina ya Scania kupinduka na kuziba barabara  katika daraja la Lwinga wilayani Namtumbo  mkoani Ruvuma.

Walionusurika kwenye ajali hiyo akiwemo kondakta wa lori hilo  lililotokea  mkoani Ruvuma likielekea jijini Dar es Salaam  Bw. Charles Ngonyani wanasema ajali hiyo imetokea wakati dereva wao haji mashaka akilikwepa lori  jingine aina ya fuso ndipo likapinduka  na kuziba  barabara.

Kondakta huyo anasema kuwa katika ajali hiyo aliyeumia zaidi ni dereva wao Haji Mashaka aliyelazwa  katika kituo cha afya cha Namtumbo  huku  yeye  na  mwenzake  Charles  Ngaponda wakipata majeraha madogo madogo.


Kwa upande wao abiria wanaosafiri  kuelekea  mikoa ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara na wanaotokea mkoa wa Ruvuma wakielekea mikoa hiyo wanaeleza adha wanayoipata kutokana  na ajali hiyo.

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma  limethibitisha kutokea kwa  ajali hiy  huku likisimamia zoezi la kuliondo lori lililoziba  bara bara.

No comments: