Advertisements

Tuesday, April 11, 2017

MBUNGE WA MTAMA MH NAPE AKUTANA NA WAZEE MAARUFU WA JIMBO LAKE KUZUNGUMZIA MAENDELEO YAO KWA PAMOJA

Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiwasili katika kikao kati yake na wazee Maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A, kikilchofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki kijiji cha Majengo A huku akiwa ameongozana na Katibu Msaidizi wa Wilaya ya Lindi Vijijini Bw. Shaibu Bakari Ngatiche .
Mbunge wa jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akizungumza na Wazee maarufu wa Kata ya Mtama na Majengo A ,katika kikao chao kilichofanyika katika ukumbi wa kaniasa la Katoliki,Mtama Lindi Vijijini.Mh Nape alizungumza mambo mengi ikiwemo na kuwaomba Wana Mtama kusameheana kwa mambo yote mabaya yaliyokuwa yametokea na kuanza ukurasa mpya wa kujenga undugu wa kupendana na kushirikiana katika mampo mbalimbali,amewaomba kuziweka kando itikadi zao za kisiasa na badala yake wakae kwa umoja wao wafirie namna ya kuliletea maendeleo jimbo la Mtama.
"Ndugu zangu,Wazee Wangu siasa kwa sasa zimekwisha,niwaombe tu,itikadi zetu za kisiasa tulizokuwa nazo tuziweke kando,tuanze upya kwa pamoja kuijenga Mtama yetu ili ipige hatua katika suala zima la Maendeleo,na mie kwa vile nimepata nafasi ya kuhakikisha jimbo la Mtama linapata maendeleo,basi ntahakikisha yale yote niliyo yaahidi wakati wa kampeni,ndani ya miaka mitano niwe nimemaliza ama kuyakupunguza kwa kiasi kikubwa",alisema Nape.Picha na MichuziJr.
 Baadhi ya wazee wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Nape Nnauye alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali ya kuhakikisha jimbo la Mtama na kusini kwa ujumla inaanza kupiga hatua kimaendeleo
 Baadhi ya akina Mama waliofika kumsikiliza Mbunge wao
 Mmoja wa Wananchi wa jimbo la Mtama akielezea moja ya changamoto ndani ya jimbo hilo,ambalo amemuomba Mh Nape alifanyie kazi
Mh.Nape akiwa katikati ya Wazee Maarufu wa jimbo la Mtama wakisubiri chakula cha pamoja
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi vijijini Bw. Mohamed Nanyali akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo hilo Mh. Nape Nnauye ili kuzungumza na wapiga kura wake kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo Wazee maarufu wa jimbo hilo. 

4 comments:

Anonymous said...

cjui boss gani atampa kazi huyu anaeonyesha kukupinga hadharani, itakuwa tabu sana, alikuwa na kazi nzuri angetulia ila ndio hivyo tena kwenye miti, sijui kalewa babake nani? mie naona ataishia ubunge tu wadhfa mwingine asahau, sorry nape you had your chance and blew it.

Anonymous said...

pole nape laiti ungejizuia ule kuku zako ingekuwa vingine.

Anonymous said...

katika watu waliobahatika huyu alikuwa mmoja wapo ila alilewa jina la nnauye, too late nape subiria 2025 kama bado uko.

Anonymous said...

huyu jamaa lazima anajuta sana saa hizi licha ya kuitwa shujaa na nini sijui aliingiliwa na nini