Advertisements

Tuesday, April 11, 2017

Mchezaji wa Kimataifa Adi Yussuf Aitaka Zanzibar Heroes Bila Kinyongo.

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya Grimsby Town ya Uingereza, Adi Yusuf ameelezea matumaini yake ya kuiwakilisha timu ya taifa ya visiwa vya Zanzibar, Zanzibar Heroes.

Katika mazungumzo na mtandao wa Soka360, Adi hakuficha furaha yake kufuatia Zanzibar kupewa hadhi ya uanachama kamili na Shirikisho la Soka barani Afrika.

”Nilifurahishwa sana kwa Zanzibar, ardhi niliyozaliwa, kukubaliwa kuwa mwanafamilia kamili wa CAF. Ni hatua nzuri kwa maendeleo ya soka la Zanzibar na ni muendelezo mzuri wa utambulisho wa fahari ya visiwa vyetu.”

”Nina matumaini itafika siku njema nitakayovaa jezi za visiwa hivyo na kuweza kuiwakilisha ardhi yangu ya asili na kuisaidia katika safari muendelezo wa safari yake ya soka la kimataifa. ”

Adi aliwahi kuitwa timu ya ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na aliyekuwa kocha wa wakati huo, Boniface Mkwasa lakini kwa bahati mbaya mechi dhidi ya Chad iliyeyuka baada ya taifa hilo kujitoa katika mechi za mchujo wa kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika.

ZANZNEWS

No comments: