Advertisements

Wednesday, April 12, 2017

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Reli ya Kimataifa

2 comments:

Anonymous said...

Vizuri sana nchi imepata kiongozi wa maana,Mungu mkubwa sana, that's real a turning point for tanzanians .Africa tatizo sio rasilimali.Africa imejaa rasilimali za aina zote kuanzia rasilimali watu mpaka hali ya hewa vyote vipo vya kutosha. Nchi nyingi za kiafrika zinakosa viongozi wenye moyo na uzalendo wa kuweka maslahi ya taifa na watu wake kwanza kuliko maslahi yao binafsi. Vile vile kuna fununu yakwamba kuna baadhi ya nchi za nje hasa zile za magharibi zinachangia au zilichangia kuhakikisha kuwa Africa inakuwa na viongozi watakaowaamua wao kwa maslahi ya mataifa yao zaidi kuliko maslahi ya waafrica, sina uhakika na hilo lakini mara nyingi lisemwalo huwa lipo na hasa ukichukulia masuala kama hayo ni kazi za makachero waliobobeya mara nyingi huletwa Africa kama mapadri,wataalam wa misaada, madaktari, vikundi vya asasi za kiraia, walimu,watumishi wa mabalozi, nakadhalika nakadhalika. Na kwa kuchukulia yakwamba ukoloni umekwisha kwa nchi za Africa lakini akili nyingi za waafrica bado zimo ndani ya ukoloni,bado zimetawalia kwa kuamini yakwamba waafrica mzungu ndio kila kitu. Hata atokee mpuuzi tu wa kizungu achukuwe begi lake akishuka tu katika nchi zetu basi anaweza kuigiza kila aina ya usanii na watu wakamuamini hata pasi ya kufuatilia back ground yake na hiyo ndio Africa yetu. Nimeanzia kueleza hayo kwa sababu napata mashaka sana na watanzania hasa wale wanaojiita wasomi kwa pande zote mbili upizani na wa chama tawala. Napata mashaka na baadhi ya watanzania wanatilia mashaka juu wa uwezo wa Maghufuli katika utendaji wake wa kazi. Napata mashaka juu ya watanzania wanaotilia mashaka uwezo wa Maghufuli katika kuiongoza nchi yetu kuelekea Tanzania mpya wakati ndio kwanza ameanza kazi na kuna kila dalili yakwamba viatu vyake hata angepewa gifted mwalimu nyerere basi kuvivaa ingekuwa shida . Maghufuli anaweza tena sio anaweza tu? Maghufuli ni very rare and gifted leader among Africans, ambae kila nchi ingetamani kuwa nae. Lakini la kushangaza na kusikitisha unaona jinsi gani baadhi ya watanzania wanavyotumia nguvu na muda na kila aina walichonacho kibaya cha kusema ili wawasibitishe walimwengu na dunia yakuwa Maghufuli hafai,jamani? Kweli sisi watanzania wanga sana na tuna roho mbaya. Au labda kama waswahili wanavyosema kunako msafara wa nyumbu basi mafisi nao wamo humo humo ndani. Maana katika kipindi kifupi cha uongozi wake muheshimiwa Maghufuli amefanya mengi na hasa ile vita yake zidi ya mafisadi hapana shaka ameshajijengea maadui wengi,wale mafisadi na makartel wa madawa ya kulevya na mitandao yao, na wale waliokuwa wakinufaika na hizo kazi zao haramu iwe rafiki,ndugu,watoto nakadhalika nakadhalika inaonekana wamekusanya nguvu zao kwa kushirikiana na wapinzani kumpiga vita raisi kwa kisingizio cha demokrasia na huo ni usaliti wa hali ya juu kwa taifa. Watanzania washukuru Mungu kwa kujaliwa kiongozi asietaka Nothing but to make his country great. Watanzania ni wavivu na raisi ameliona hilo na ndio maana anahimiza watu wafanye kazi badala ya kulilia tu, watanzania wengi wetu si waadilifu na ndio maana raisi amekuwa mkali kiasi kwamba wakati mwengine anaamua yeye mwenyewe binafsi kwenda kwenye site kuangalia uadilifu wa kazi ukoje. Watanzania wengi wetu ni waoga "sio wakutukana" bali wakujaribu mambo ya maana ya maendeleo pamoja na kukabiliana kiushindani wa kiutendaji na watu wa mataifa mengine na ndio maana muheshimiwa raisi anasema kwa kujiamini yakuwa Tanzania ya viwanda inawezekana lakini wapo wanaocheka chini chini na wanaosema hadharani yakwamba haiwezekani kwa kweli muheshimiwa raisi anachallenge kubwa sana na Mungu atamsaidia. Ila watanzania wengi tunaimani muheshimiwa raisi hata tetereka na tunakuomba shikilia Uzi huo huo na hata kama utazidisha ukali zaidi itakuwa powa sana,Mungu akuweke baba na dhidi kuwaelimisha watanzania walio wema wa kawaida yakwamba kila ndoto njema wanayoiwaza ya maendeleo yao na familia zao basi wakati umefika,wakati ndio huu wa kutimiza hizo ndoto kwa vitendo na hapana shaka zitatimia kutokana na kuwa na serikali adilifu ya awamu ya tano.

Anonymous said...

Hiyo Ni Reli ya Kimataifa au reli ya kati itakayotoa huduma kati ya Dar - Moro na baadae Dodoma. Mbona mnapotosha na kutokuwa wakweli! Kuna umataifa gani hapo. Haiwezi kuhudumu Mikoa zaidi ya mitano na bado tunaita ya Kimataifa!!