Advertisements

Tuesday, April 18, 2017

TAASISI YA NAMELOK KUJENGA KITUO CHA ELIMU KWA AJILI YA WAJASILIAMALI WASICHANA WILAYANI KIBAHA MKOANI PWAN

 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia  Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo kata ya Mwendapole na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet Mwasuka wa  kushoto ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasicahna na wanawake wajasiriamali  waliopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kulia Happiness Seneda kulia akiwa amemshika mmoja wa watoto huku akisikiliza maelekezo kuhusina na ujezni wa kiutuo hicho maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichan na wakinamama kinachijengwa katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok Janet Mwasuka.
  Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Nameloc akoinyesha eneo ambalo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichana na wanawake wajasiriamali katika kata ya Mwendapole  Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo maalumu cha wasichana  na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa kinajihusisha na masuala ya  utoaji wa mafunzo  mbali mbali kwa lengo la kuweza  kuwapa fursa ya  kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao wenyewe.

Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika katika Kata ya Mwendapole  iliyopo  katika halmashauri ya mji wa Kibaha  Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika kwa ujenzi  huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake  hao kiuchumuni  kupitia  mafunzo ya stadi za kazi pamoja na  fursa zilizopo  kutokana na elimu watakayoipata.

Janet alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini Dar es Salaam inayojishughulisha na  kuwasaidia katika kuendesha biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali  Hilda Kisoka  amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na kuuza bidhaa  wanazozizalisha hapa nchini  hadi nje ya nchi kwa lengo la kujitangaza zaidi.

Alisema kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika kuleta ushindani zaidi  wa masoko katika nchi zingine za nje na kuondokana na kuwa tegemezi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani amekemea vitendo vya wanawake kufayiwa vitendo vya ukataili na unyanyasaji na  kujikuta  baadhi yao wanashindwa kutimiza ndoto  zao na malengo yao waliyojiwekea katika siku za baadae.

“Jamani mimi mwenyewe nimeshuhudia baadhi ya maeneo kuna watu wanafanya vitendo vya ukatili na kuwanyanyasa wanawake yani hili suala kwa upande mimi kwa kweli silipendi kwa sababu baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza malengo yao ambayo yamejiwekea kwa hiyi katika hili sisi kama serikali ni lazima tulivalie njuga ii kuondokana na hali hii,”alisema Seneba

Pia katika hatua nyingine alitoa wito kwa wakinababa wote katika Mkoa wa Pwani kuachana na vitendo hivyo vya kuwanyanyasa wanawake na kuwapiga bila sababu zozote za msingi na badala yake wabadilike na kuhakikisha kwamba wanawasaidia kuwawezesha katika shughuli zao mbali mbali za ujasiriamali  kwa lengo la kuweza kupambana na  wimbi la umasikini.


KITUO hicho ambacho kinajegwa katika kata ya Mwendapole kinatarajiwa mpaka kukamilika kwake kugharimu kiasi cha shilingi milioni 45  na katika awamu ya kwanza  kinatarajia kuwanufaisha wanawake  wapatao 200 kutoka Wilayani Kibaha mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine ya jirani ambao watapatiwa mafunzo  mbali mbali ya ujasiriamali.

No comments: