Advertisements

Wednesday, April 12, 2017

Taiwan yapiga marufuku ulaji wa mbwa na paka

Bunge la Taiwan, limeidhinisha mswaada wa kupiga marufuku uchinjaji wa paka na mbwa, kwa matumizi ya binadamu.
Mswaada huo pia unazuia wale wanaotumia gari au pikipiki kuwavuta wanyama wao wa kuchezea, au kuwatanguliza wanaposafiri.

Yeyote atakayepatikana akikiuka amri hiyo, atakabiliwa na faini kubwa au kufungwa hadi miaka miwili jela - na majina pamoja na picha zao kuwekwa hadharani.
Hatua hiyo imeanzishwa ili kuboresha sheria za kuwalinda wanyama nchini humo.
Bunge la Taiwan, limeidhinisha mswaada wa kupiga marufuku uchinjaji wa paka na mbwa, kwa matumizi ya chakula cha binadamu


Bunge la Taiwan, limeidhinisha mswaada wa kupiga marufuku uchinjaji wa paka na mbwa, kwa matumizi ya chakula cha binadamu
Hatua hiyo ya Jumanne wiki hii, ni mabadiliko makubwa mno ya kuwalinda wanyama nchini Taiwan, na ni moja ya aina yake kuanza kutekelezwa barani Asia.
Mwaka 2001, Taiwan ilipitisha sheria ya kupiga marufuku uuzaji wa nyama na manyoya ya wanyama wa kuchezea kama vile paka na mbwa, kwa kile kilichotajwa "madhumuni ya kiuchumi".
Nyama ya mbwa, zamani ilitumika kwa mara katika kisiwa hicho kama chakula, lakini kwa sasa mnyama huyo anafaa kujumishwa kama mmojawepo wa wanafamilia.

BBC SWAHILI

No comments: