Advertisements

Monday, July 31, 2017

Mbowe apinga wawekezaji kunyang'anywa viwanda

By Peter Elias, Mwananchi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Serikali haiwezi kujenga viwanda pekeyake bila kuihusisha sekta binafsi ambayo ndiyo mdau mkuu katika uwekezaji nchini.

Mbowe amepinga kusudio la Rais John Magufuli kuwanyang'anya wawekezaji viwanda walivyobinafsishiwa kwa madai kwamba Serikali ilitakiwa kutafuta chanzo cha kufungwa kwa viwanda hivyo kabla ya kufikia uamuzi wake.

Mwenyekiti huyo amebainisha sababu mbalimbali zilizofanya viwanda hivyo visifanye kazi kuwa ni pamoja na kutopatiwa ruzuku na Serikali, teknolojia ya zamani ya viwanda hivyo na wakati viwanda hivyo vinajengwa kulikuwa na mfumo hodhi wa soko.

"Hakuna mfanyabiashara duniani àmbaye atapewa kitega uchumi kinachozalisha halafu akakifunga. Hayupo!" amesema Mbowe.

Amesema Rais Magufuli hana mapenzi na sekta binafsi kwa kuwa anaamini kwamba kila mtu aliye kwenye sekta binafsi ni "mpiga dili."

1 comment:

Unknown said...

Mbowe we fikiria au chunguza kwanza Kabla ya kulaumu serikali ..