Advertisements

Thursday, July 20, 2017

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AHIZIMIZA USHIRIKIANO KUKABILI UKATILI DHIDI YA ALIBINO

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. George Masaju akimsikiliza Bi. Ikponwosa Ero, Mataalam Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albnism. Mhe. Mwanasheria Mkuu na Bi. Ero walikutana leo Jijini Dar es Salaam, ambapo walibadishana mawazo kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inavyoshughulikia matukio ya kijinai dhidi ya watanzania wenye albnism.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akifafanua kuhusu namna Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Divisheni ya Mashtaka inavyoshughulikia kwa kupeleleza na kuendesha kesi za jinai dhidi ya watu wenye albnism. katika maelezo yake Mwanasheria Mkuu amesema Serikali inachukulia kwa uzito wa hali ya kipekee matatizo yanayowakabili watanzania wenye ualbino na kwamba juhudi hizo zimesaidia sana katika kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya jinadi dhidi ya watanzania hao ingawa bado kunachangamoto.

Na Mwandishi Maalum, Julai 19,2017


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju ametoa wito kwa Asasi zisizo za kiserikali ( NGO) kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupitia ushirikiano huo kukomesha na hatimaye kumaliza kabisa changamoto zinazowakabili watanzania wenye albinism.

Mwanasheria Mkuu ametoa wito huo leo ( Jumatano)wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Bi Ikponwosa Ero, Mtaalamu Huru wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wenye albinism

“ Ningependa kutoa shukrani zako kwa kuamua kuja Tanzania na kukutana na viongozi mbalimbali wa Serikali, hii ni fursa muhimu kwako ya kupata taarifa sahihi na rasmi kuhusu jitihada , juhudi na mikakati mbalimbali inayofanywa na serikali na taasisi zake katika kukabili vitendo vya jinai dhidi ya watanzania wenzetu wenye albinism” akasema Mhe. Mwanasheria Mkuu

Na Kuongeza “ kupitia kwako nikuombe basi uwahimize viongozi wa asasi zisizo za kiserikali hususani zile zinazojihusisha na watanzania wenye albinism kushirikiana na kufanya kazi kwa karibu na Ofisi yangu na Taasisi nyingine za serikali kwa sababu wote tuna nia na lengo moja la kuwasaidia watanzania wenzetu”..

Akasema Serikali inachukulia kwa uzito wa hali ya juu makosa ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism na kwamba, watuhumiwa wote ambao wamepatikana na hatia wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na sheria kuchukua mkondo wake.

Akasisitiza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesisitiza sana juu ya haki ya mtu kuishi na kwamba haki hiyo ni kwa watanzania wote bila ya kubagua wakiwamo watu wenye albinism au ulemavu wa aina yoyote.

“ Haki ya mtu kuishi imefafanuliwa na kuelezwa kwa kina kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na haki hiyo haimbagui mtu mwenye albinisim au mtanzania yoyote ile na ndio maana makosa ya jinai dhidi ya haki ya mtu kuishi awaye yeyote yule yanachukuliwa kwa uzito ule ule”.

Kuhusu takwimu zinazohusu matukio ya jinadi dhidi ya watanzania wenye albinism,Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kwamba tangu mwaka 2006 hadi mwaka huu kumekuwa na matukizo 66 dhidi ya watu wenye albinisma na huki miaka mingine ikiwa na haina tukio lolote lile na kwamba kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali matukio hayo yameendelea kupungua kwa kiasi kikubwa sana mwaka hadi mwaka.

Kuhusu hukumu dhidi ya watuhumiwa, Mwanasheria mkuu amesema utekelezaji wa hukumu dhidi ya watuhumiwa wa makoja hayo ya jinai umekuwa wa mafanikio makubwa kwa zaidi ya asilimi 90 na kwamba hukumu zilizotolewa ni pamoja na vifungo, huku ya kifo kwa baadhi ya watuhumiwa. Ingawa pia kuna walioachiwa huru kutoka na kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametaja baadhi ya mafanikio mengine ni pamoja na Ofisi yake kuandaa na kutekeleza uratibu wa uhuishaji wa takwimu za matukio ya kijinai dhidi ya watu wenye albinism. Uratibu ambao ulifanyika mwaka 2014 kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Sheria na Katiba na Asasi za Kiraia.

Aidha ametaja mafanikio mengine ni kuanzishwa kwa dawati maalum katika Divisheni ya Mwendesha Mashtaka kuhusu watu wenye albinism, kusimamia upepelezi na kuendesha kesi.

Kwa upande wake Bi. Ikponwosa Ero akielezea madhmuni ya ziara yake hiyo hapa nchini kuwa , pamoja na mambo mengine, kutathimini hali ya haki za bindamu za watu wenye albinisma,, kutathimini hatua na jitihanda zinazofanywa na Serikali katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili watu wenye albinism, kubainisa mapungufu na kuona uwezekano wa kuziba mapengo ya mapungufu hayo.

Pamoja na kuuliza maswali mbalimbali kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , maswali na hoja zilizojibiwa na Mwanasheria Mwenyewe, pamoja na Mkurugenzi wa Divisheni ya Katiba na Haki za Binadamu na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Divisheni ya Mashtaka, Mtaalamu huyo amemshukuru Mwanasheria Mkuu kwa kutenga muda wa kukutana naye na kwa maelezo na taarifa zikiwamo za kitakwimu ambazo zimewasilishwa kwake. Pamoja na kutambua juhudi za serikali katika eneo hilo.

Bi. Ikponosa Ero aliteuliwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa June 15, 2015 kuwa Mtaalamu Huru wa haki za bindamu kwa watu wenye albinism.


Imetolewa na Kitengo cha Mwasiliano
Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali
Dar es Salaam

No comments: