Advertisements

Thursday, July 27, 2017

NANDO AWA FITI, AITWA MAREKANI

MSHIRIKI wa Big Brother 2013, Nando Khan ambaye hivi karibuni alikuwa ameathirika kwa matumizi ya madawa ya kulevya, kwa sasa yupo fiti na muda wowote anaweza kuondoka Tanzania kwenda Marekani baada ya familia yake kuanza harakati za kumtafutia hati ya kusafiria ‘visa’ kwa ajili ya kwenda kuishi huko.

Nando amerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kuwa chini ya uangalizi wa Kituo cha Kuzia Matumizi ya Madawa ya Kulevya cha Pillimissana Foundation kilichopo Kigamboni, Dar.

Akizungumza na gazeti hili mkurugenzi wa kituo hicho, Pilli Missana, alisema: “Nando amebadilika sana na yuko tofauti na hapo awali, hivi tunavyoongea, wazazi wake wapo kwenye harakati za kumtafutia hati ya kusafiria ili aende kuishi Marekani na kuondoka kabisa kwenye mazingira ambayo yamesab-abisha kuwa vile alivyo-kuwa awali.”

IMELDA MTEMA | GAZETI LA AMANI

No comments: