Advertisements

Wednesday, August 2, 2017

MWENYE SIMU HAKOSI NAMBA!

WAHENGA wanasema sahani iliyofunikwa, kilichomo kimesitirika! Basi kama hujanielewa utanielewa nikimaliza makala haya, upo? Ni Jumanne nyingine shoga yangu tunakutana tena kwenye kona yetu ya kujidai, kona ya kukuhabarisha kama siyo kukuelimisha!

Kona hii kama ada kunyoosha tabia za watu wanaojifanya wameshindwa kunyooshwa! Huu dada ni muarobaini unatibu magonjwa zaidi ya elfu moja, lazima la kwako litakuwemo. Kwangu si lazima nikufikie, kuona kwako ndiko kupona kwako!

Usije kusema naongea sana na kuwanyima uhondo japo kwa wengine huwa shubiri ambayo akiimeza lazima afumbe macho na akifumbua keshapona huyo, hee hee heiiiya, kaaooogeeee!

Jamani mashostito wangu ambao hamna wapenzi najua jinsi gani mnavyoitafuta pesa kwa nguvu nyingi na siku moja mnataka kupumzika na kula raha na wenzi wenu.

Najua mnapenda kutumia pesa zenu kwa kutafuta mwanaume ambaye atakuwa chini ya miliki zenu kwa kumiliki haki zake zote kwa vile hupendi karaha unataka kula raha baada ya kuzitafuta kwa muda mrefu au mjane ambaye bado damu inachemka na anataka kuwa na mtu mwenye staha zake.

Furaha yenu ni kumtafuta mtu anayejiheshimu hata ukiwa umemzidi umri kikubwa heshima. Lakini baadhi yenu tumekuwa tukitafuta vijana wa kustarehe nao wakati huohuo tuna bwana mwingine ambaye ndiye anayeingiza kipato.

Kwa vile kijana uliyenaye umemmiliki kwa asilimia kubwa unakuwa humheshimu kwa vile kila kitu unampa na kusahau kitu muhimu kuliko vyote hapati kwako nacho ni heshima.

Wengine hudiriki kuwatukana wapenzi wao kwa vile tu wana pesa ambayo huamini ndiyo inayomuweka kwako na kusahau utu ni bora kuliko mali.

Hapa ndipo paliponifanya nizungumze na ninyi mashostito wangu. Jamani kuwa na pesa bado hakuondoi uanamke wetu na kufikia hatua ya kuwageuza wanaume tunaowamiliki kuwa wanawake na sisi ndiyo wanaume.

Shoga hata siku moja mwenye simu hakosi namba, la na masikio hayazidi kichwa, siku zote bado tutatangulia chini kwa vile ndiyo maumbile tuliyoumbiwa. Hivyo basi uanamke wetu hautabadilika kwa vile tuna pesa au tuna uwezo wa kumiliki mwanaume.

Hebu tuuheshimu uanamke wetu hata tunapozungumza na wapenzi wetu tunaowamilimiki turudi kwenye uanamke wetu hata tunapozungumza nao turudi chini siyo kuwapanda juu kwa vile tuna fedha.

Kwa mtindo huo tutakuwa mung’unya kuharibikia ukubwani, kwani ni aibu mtu mzima kuwa mama huruma kwa kubadili wanaume.

Jamani kama hukutosheka katika ujana wao utatosheka uzeeni? Hebu basi kama kweli tumeamua kumtafuta mtu ili tutulie naye basi tunatakiwa kujiheshimu na kumheshimu uliyemtafuta kwa wewe

kuwa mwanamke na yeye mwanaume.

Namalizia kwa kusema Mungu alituumba kuwa chini ya wanaume tuna haki ya kujitetea pale panapostahili hata kudai talaka lakini si kuwadharau wanaume kwa vile tuna uwezo mkubwa wa kifedha na kukua masikio kuzidi kichwa.

Sifa ya mwanamke ni unyenyekevu kwa kuamini
utu ni bora kuliko mali. Mali inaisha lakini utu wa mtu hauishi.
Kwa leo niishie hapa. Maoni na ushauri nicheki kwa namba yangu, tuma meseji tu 0713 76 11 35.
Love Life | Mapenzi & Maisha (Chumbani Zaidi) GPL

No comments: