Advertisements

Tuesday, August 1, 2017

SIMBA SC YAZINDUA WIKI YA SIMBA (SIMBA WEEK) KUELEKEA TAMASHA LA SIMBA DAY

Klabu ya Simba leo imezindua  rasmi wiki yake ijulikanayo kama (Simba Week) kuelekea kilele cha Maadhimisho ya sherehe kubwa ya timu hiyo inayofanyika kila mwaka ambayo ni maarufu kama Simba Day Hii itakuwa ni mara ya pili kufanyika  kwa Simba Week kama muongozo kuelekea Simba Day, ambapo kwa mara ya kwanza klabu hii kubwa nchini Tanzania ilizindua Simba Week mwaka jana (2016).
 Simba Sports Club inataka kujenga  ushirika mkubwa kabisa katika maeneo yote nchini kwa kushiriki katika matukio na shughuli mbalimbali za kijamii zinazolenga kurudisha kwa Jamii inayoizunguka kwa kuangalia maeneo yenye uhitaji ambapo viongozi,wachezaji, wanachama, wapenzi na mashabiki huungana kwa pamoja ili kutoa mchango wa hali na mali kwa Jamii yake kwani Simba ni Chapa (Brand) kubwa nchini na kwingineko Afrika na dunia kwa ujumla hivyo ushiriki wake kijamii una umuhimu mkubwa sana.
Simba Week  itaadhimishwa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo;
Kitembelea watoto yatima 
Kutembelea watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo 
Kugawa mipira kwenye kliniki 
Kampeni ya mtaa kwa mtaa 
Wachezaji kuongea na mashabiki 
Kukaribisha timu nyumbani 
Kupiga picha na kombe 

Kikosi cha Simba ambacho sasa wameweka kambi mjini Johannesburg, Afrika Kusini, wanatarajia kucheza mchezo wao wa kwanza wa kirafiki leo dhidi ya Orlando Pirates katika maandalizi ya Simba Day  Maandalizi ya Simba Day 2017 yanaendelea  kupamba moto ambapo kauli mbiu ya Simba Day 2017 ni "KiSimba Zaidi".Tiketi za Simba Day zitaanza kuuzwa Agosti 4 ambapo watakao nunua kuanzai tarehe hiyo hadi Agosti 7 watapata punguzo la bei wakati watakaonunua Siku ya Simba Day watapata tiketi kwa bei ya juu zaidi. Hivyo tunawaomba wanachama, wapenzi na mashabiki wote wa Simba wanunue tiketi mapema kwa bei nafuu kabisa.
Simba wamesema kuwa taarifa zote rasmi kuhusiana na klabu zitaendelea kupatikana katika chanzo cha klabu (SIMBA APP), hivyo wanahabari wawe makini na tetesi za mitaani kwani mahali pekee pa uhakika pa kupata habari za Simba ni kupitia Simba App. 
Afisa Habari Mkuu wa Simba, Haji Manara amesema kwamba kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali nchini watafanya mambo mengi ikiwemo yaliyoorodheshwa hapo awali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group ambao ni wabia wa Simba kwenye masoko na biashara alisema "Simba Day na Wiki zimekuwa sherehe muhimu zikihusisha shughuli za kurudisha kwa Jamii na kuifanya Simba iwe karibu zaidi na wapenzi na mashabiki wake.

Simba inaamini katika kujenga chapa yake kupitia shughuli za kijamii na mikakati ya kimasoko na kuwa karibu na mashabiki na wapenzi wake

No comments: