Advertisements

Monday, February 19, 2018

Rais Magufuli amemteua Prof. Makenya Maboko kuwa Mwenyekiti wa COSTECH

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH).

Uteuzi wa Prof. Maboko unaanza leo tarehe 19 Februari, 2018.

Pro. Maboko ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Februari, 2018

No comments: