Advertisements

Thursday, April 26, 2018

MWAMBATA JWTZ WA UBALOZI WA TANZANIA, INDIA APANDISHWA CHEO NA KUWA BRIGEDIA JENERALI

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka H. Luvanda akimvalisha cheo cha Brigedia Jenerali A.S Mwami ambaye ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.Brigedia Jenerali A.S Mwami ni miongoni mwa Maafisa Wakuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania ambao Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliwapandisha vyeo tarehe 12 Aprili, 2018. Awali Brigedia Jenerali Mwami alikuwa na cheo cha Kanali. Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuhudhuriwa na watumishi wa ubalozi huo.
Brigedia Jenerali Mwami akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake.
Balozi Baraka Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami
Balozi Luvanda pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.

No comments: