Advertisements

Tuesday, April 24, 2018

TANZANIA NA ISRAEL KUANGALIA NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA MASUALA YA SHERIA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akiwa katika mazugumzo na Waziri wa Sheria wa Israel Bi, Aylet Shaked. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimatifa wa Julius Nyerere ( JNICC) jijini Dar es Salaam, viongozi hao walikubaliana kwamba Tanzania na Israel zinayo maeneo ambayo kila nchi inaweza kujifunza kutoka kwa mwenzie hususani katika eneo la utoaji haki na usimamiaji wa sheria na kwamba kuna haja kupitia kwa Wanasheria Wakuu wa Serikali wa nchi hizo mbili kukutana ili kujadiliana maeneo ya kushirikiana. Waziri wa Sheria wa Israel yupo nchini akiongoza ujumbe wa wafanyabiashara. ( picha na Ofisi ya AG)
Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amekutana na kufanya mazugumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Said Hassan Said. Katika mazungumzo yao viongozi hao wamebadilishana mawazo ya namna ya kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku yanayosimamia masuala ya sheria na utaoaji haki. Pichani Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Bw. Said Hassan Said akimkabidhi Dk. Adelardus Kilangi Katiba ya Zanzibar ( picha na Ofisi ya AG

No comments: