Advertisements

Tuesday, May 22, 2018

SERIKALI YAWATAKA WADAU WA NGOs KUENDELEA KUTEKELEZA SERA ZILIZO CHINI YA IDARA KUU MAENDELEO YA JAMII

  Mkurugenzi na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katemba akizungumza na wadau  Mashirika yasiyo ya Kiserikali  yanayotekeleza Sera zilizo chini ya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bi Tausi Mwilima (kulia) akieleza yatokanayo na kikao kilichopita kati ya Serikali na wadau wa NGOs wanaotekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii  Jijini Dodoma.
 Mwakilishi kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi Janeth Edson akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa hati ya makubaliano ya utekelezaji wa Sera mbalimbali baina ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi akitoa mrejesho wa maendeleo ya utekelezaji wa hati ya makubaliano na ushirikiano kati ya wadau wa NGOs baina ya Serikali na NGOs kwa upande wa Serikali katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa mpango wa kuamsha ari ya wananchi kujitolea katika shughuli za maendeleo kwa wadau wa NGOs katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto Bi. Grace Mwangwa akitoa mrejesho kuhusu utekelezaji wa makubaliano na wadau kuhusu utekelezaji wa Sera ya Mandeleo ya Mtoto kwa wadau wa NGOs katika kikao kati ya Serikali na wadau hao Jijini Dodoma.  
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kati ya Serikali na wadau wa NGOs Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi wetu Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeawataka wadau wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuendelea kutekeleza Sera mbalimbali zilizo chini ya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii katika utekelezaji wa majukumu yao.

Hayo yamesemwa Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi na Msajili wa NGOs Bw. Marcel Katemba Jijini Dodoma wakati wa  Kikao kati ya Serikali na Wadau hao kinachokaa kwa siku moja kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi zao na kutekeleza Sera zilizo chini Idara kuu Maendeleo Jamii.

Ameongeza kuwa katika kutekeleza Sera mbalimbali Serikali inashirikiana na Wadau mbalimbali wa maendeleo nchini ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.

Amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanafanya kazi kubwa nchini katika kuleta maendelo ya jamii na Taifa katika sekta mbalimbali nchini.

“Wadau wa NGOs mnafanya kazi nzuri na kubwa katika kuleta matokeo chanya kwa jamii na taifa letu” alisisitiza Bw.Katemba.

Kwa upande wake Mwakilishi Kutoka Shirika la World Vision Tanzania Bi. Janeth Edson akitoa mrejesho wa makubaliano kati ya Serikali na NGOs kwa upande wa NGOs amesema kuwa wao kama wadau wataendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Sera mbalimbali na kuwaasa wadau kuendelea kuunganisha nguvu na Serikali katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo.

No comments: