Advertisements

Friday, June 22, 2018

Washiriki Washinda Vikombe, Fedha Maonesho ya Utumishi wa Umma Muhimbili

 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya kikombe kwa Idara ya upasuaji ambayo imekuwa mshindi wa kwanza kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yalianza tarehe 18 hadi 20 Juni, 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili.  Idara hiyo imepatiwa zawadi ya kikombe, fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akishuhudia shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washiriki mbalimbali. Mwenyekiti huyo amefunga maonesho ya siku tatu yalioanza tarehe 18 hadi 20, Juni 2018 kwenye viwanja vya Muhimbili. Wengi walijitokeza kupima afya BURE, kupata elimu na ushauri kuhusu afya zao.
 Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali, Dkt. Juma Mfinanga akipokea zawadi ya kikombe kutoka kwa Prof. Majinge. Pia, Idara hiyo imepatiwa fedha na cheti cha ushiriki. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru.
 Wananchi wakitembelea banda la Magonjwa ya Damu na Saratani za Damu katika maonesho yaliofanyika Muhimbili.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akikabidhi zawadi ya fedha na kikombe kwa Idara meno.
 Idara ya macho nayo haikuwa nyuma katika kutoa huduma bora kwa wananchi waliofika kwenye banda lao kwani walishinda kikombe pamoja na feda taslimu.
 Wananchi wakisubiri kuhudumiwa katika banda la lishe kwenye maonesho hayo.
 Mkuu wa Kitengo cha Lishe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Schola Mlinda akipokea zawadi baada ya kuwa mshindi wa tano.
 Wananchi wakiwa kwenye banda la Idara ya Magonjwa ya Kinamama na Uzazi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof.  Majinge akiwa kwenye banda la lishe. Kushoto ni Mtaalamu wa Lishe, Mariam Nyamwaira akimsikiliza mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Charles Majinge akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa maonesho hayo.

No comments: