Advertisements

Thursday, August 9, 2018

RAIS MAGUFULI AONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUAGA MWILI WA MAREHEMU MZEE AMRI ATHUMAN ‘KING MAJUTO’ LEO JIJINI DAR ES SALAAM

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa heshima za mwisho katika jeneza lenye mwili wa Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimfariji Hamza Amri Athuman mtoto wa marehemu Msanii mkongwe wa Vichekesho na Maigizo nchini Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally akisoma dua kumuombea Marehemu Mzee Amri Athuman “King Majuto katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mara baada ya dua hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliongoza mamia ya wananchi kutoa heshma za mwisho katika msiba huo. PICHA NA IKULU

No comments: