Advertisements

Tuesday, October 16, 2018

UN, Serikali wazungumza na vijana

 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba katika bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigella.
Sehemu ya vijana kutoka shule mbalimbali pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali walioshiriki bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
 Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
 Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama akikabidhi medali kwa timu za vijana walioshiriki michezo mbalimbali wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge. Kushoto ni Waziri wa Vijana, Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume.
 Baadhi ya makundi mbalimbali ya vijana wakishiriki mchezo wa kuvuta kamba wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
 Vijana kutoka maeneo mbalimbali wakishirikishi soka wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
 Vijana wakishiriki mchezo wa kukimbia na magunia wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Baadhi ya wanafunzi wakipozi na mabango ya malengo ya maendeleo endelevu wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano UNESCO, Nancy Kaizilege katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali wakiwa wameshika mabango ya malengo ya maendeleo endelevu wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Wanafunzi wakifurahia mara baada ya kushiriki michezo mbalimbali wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Vijana, Utamaduni,Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mh. Martine Shigella katikati picha ya pamoja na vijana walishiriki michezo mbalimbali wakati wa bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
SERIKALI ya Tanzania ikishirikiana na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa wamefanya tamasha kubwa la vijana mjini Tanga, mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana nchini Tanzania.
Tamasha hilo ambalo lilishirikisha vijana 500 limewezeshwa na mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa ya UNESCO, UN Women na UNFPA kwa kushirikiana na Serikali.
Katika tukio hilo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) Balozi Ali Abeid Aman Karume. Tamasha hilo liliwakumbusha vijana ushiriki wao katika malengo ya dunia kupitia michezo ukiwamo soka.
Wakiwa na wito wa nafasi salama ya vijana, michezo imetumika katika kushawishi vijana kujieleza na kuimarisha uwezo wao wa kimichezo ili kuchangia utekelezaji wa malendo endelevu ya dunia.
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Desemba 2013 lilipitisha Aprili 6 kuwa siku ya michezo kwa maendeleo na amani.
Siku hiyo huadhimishwa kwa kuwaleta pamoja watu wengi katika michezo kama sehemu ya kuwa na amani, kutengeneza uvumilivu na heshima.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Jenista Mhagama, amewataka vijana kutambua wajibu wao na kutekeleza mipango endelevu ya nchi huku wakijihakikishia usalama wao.
Waziri Mhagama alitoa kauli hiyo kwenye bonanza la wiki ya vijana lililofanyika jijini Tanga na kudhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) kuelekea kilele cha mbio za Mwenge.
Aidha alirejea ujumbe wa Mwenge mwaka huu ambao umesisitiza mapambano ya Ukimwi, Malaria na matumizi ya dawa za kulevya na mapambano dhidi ya ufisadi kwa Tanzania.
Alisema mpango shirikishi wa malengo ya Dunia wa mwaka 2020 unalenga kusaidia vijana kupima afya zao, kupatiwa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi huku serikali kupitia mamlaka zake zikipambana kudhibiti maambukizi mapya.
Mhagama alisema Taifa lina idadi kubwa ya vijana, hivyo ikiwa uzalendo, nguvu na nafasi waliokuwa mnayo vikitumiwa vizuri wanaweza kuwa na mchango mkubwa wa ujenzi wa uchumi wa nchi.
Awali Mkuu wa Kitengo cha Habari na  Mawasiliano UNESCO, Nancy Kaizilege alisema ipo haja ya kuangaza uwezo wa vijana katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo.
Alisema vijana wanahitaji kuungwa mkono kutokana na mchango wao katika nchi na ulimwengu kwa njia wanazoamua kupitia, ili kufanikisha malengo yao bila kujali njia gani wanatumia.

No comments: