Advertisements

Sunday, December 9, 2018

LUANGISA AFRICAN GALLERY MAMBO YALIKUWA MOTO MOTO


Luangisa African Gallery ilikuwa imeandaliwa na Rose Luangisa mama wa Kitanzania anaeutangaza utamaduni wa Tanzania hapa New York, Marekani kwa kufanya Biashara ya Vinyago na nakshi nakshi nyingi zenye asili ya Tanzania. Hapa Mayor Richard Thomas wa Mt Vernon New York akikabidhiwa fimbo ya heshima na Mh. Modest Mero, Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Hawa wote walipata nafasi ya kukaribishwa katika maonesho haya yaliyokuwa kivutio kwa kuonesha ni kihasi gani Nchi yetu ya Tanzania ilivyokuwa na hazina kubwa ya vivutio vya kiasili.


Rose Luangisa akitoa maelezo ya kila kitu kinachopatika katika maonesho hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mt Vernon New York Rose ufanya maonesho kama haya mara kwa mara na kukaribisha watu mbalimbali. Kwa taswira zaidi nenda chini.

Mh. Balozi akionesha ufundi wa kupiga banjo kama unavyoona alipiga kwa ufundi kabisa hadi alisababisha Mayor kusinzia. Balozi Mero ni mtu wawatu na tunajivunia kuwanae New York kwani ni  mchapa kazi na kiongozi anaejitoa kwa kila jambo yeye pamja na mama mwenye nyumba wake.





No comments: