Advertisements

Thursday, March 21, 2019

MAALIM SEIF, ZITTO KABWE WATUA ZANZIBAR

KIONGOZI wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe akiambatana na Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi na wanachama wengine wamewasili katika ofisi za chama hicho zilizopo Vuga, Mjini Unguja leo Machi 21, 2019.

Zitto amewasili katika ofisi mpya za ACT- Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja ambazo awali zilikuwa makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF) visiwani humo.
Baada ya kuwasili katika ofisi hizo , Maalim Seif alimpokea Zitto huku mamia ya wana ACT- Wazalendo wakimpokea kwa nyimbo mbalimbali.
Zitto na Maalim walivalishwa mataji na baadae wakamwagiwa mchele ambapo wenyeji wanasema tafsiri yake ni kuwaepusha na husda na jicho baya, kisha wakaenda kukaa eneo maalum lililoandaliwa GPL

No comments: