Advertisements

Saturday, June 22, 2019

FIRST LADY NA MAKAMU WA RAIS DMV WANADI KONGAMANO LA WANAWAKE VOA

 Mkuu wa idara idhaa ya Kiswahili Sauti ya Amerika (VOA) Dkt. Hamza Mwamoyo akipata picha akiwa ofisini kwake siku ya Ijumaa June 21, 2019 siku Vijimambo Blog ilipotembelea jengo la Radio na Luninga idhaa ya Kiwahili na kujionea utendaji kazi wa waTanzania hao jinsi gani wanavyochapa kazi.
 Kushoto ni makamu wa Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bi. Joha Nyang>anyi na first Lady wa Jumuiya Bi. Gloria Alex wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa idara ya idhaa ya Kiswahili (VOA) Dkt. Hamza Mwamoyo walipokutwa na kamera ya Vijimambo Blog  walipokwenda kunadi Kongamano la wanawake litakalo fanyika leo Jumamosi June 22, 2019 Gaithersburg, Maryland kuanzia saa 11 jioni.
 Matangazaji Mary Mgawe (kulia) akiwaelekeza jambo first Lady  Gloria Alex na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bi. Joha Nyang'anyi siku ya Ijumaa June 21, walipokua wametembelea idhaa hiyo kunadi usiku wa kongamano la wanawake litakalofanyika leo Jumamosi June 22, 2019Gaithersburg, Maryland.
 Mtangazaji Mary Mgawe akijiandaa kurusha kipindi cha Luninga pendwa kote ulimwenguni cha Duniani Leo kinachorushwa  mbashara kuanzia saa 2 asubuhi saa za Amerika ya Mashariki.
 Kutoka kushoto ni first lady Gloria Alex, Makamu wa Rais Jumuiya ya waTanzania DMV Bi. Joha Nyang'anyi wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa idara ya idhaa ya Kiswahili Sauti ya Amerika (VOA) Dkt. Hamza Mwamoyo ndani ya studio ya luninga.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

 Kutoka kushoto ni first Lady Gloria Alex, Dkt. Hamza Mwamoyo,Mary Mgawe na Makamu wa Rais Bi. Joha Nyang;anyi.

 Mtangazaji nguli wa Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili Bi. Khadija Riyami (kati) akifanya mahojiano na first Lady Bi. Gloria Alex (kushoto) na Makamu wa Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV siku ya Ijumaa June 21, 2019 siku first lady na makamu walipotembelea idhaa hiyo kunadi kongamano la wanawake litakalofanyika leo Jumamosi June 22, 2019 Gaithersburg, Maryland.
Bwn. Omari Kaseko akiandaa kipindi cha Duniani Leo mapema asubuhi ya siku hiyo.
 Bi. Radhia Adam akijiandaa na akitayarisha habari za kipindi cha Duniani Leo.
 Bi. Honeymoon Al Jabir akiwa kwenye matayarisho ya mwisho ya kipindi cha Duniani Leo asubuhi na mapema.
 Fundi mitambo wa Radio idhaa ya Kiswahili Bwn.Binj Murithi akiwa yupo tayari kuelekea studio namba 42.
 Bwn. Jaffar Mriha akiwa ofisini kwake.
 Bi. Khadija Riyami akiandaa taarifa mbalimbali kwa ajili ya kipindi.
 Bi. Mkamiti naye akikusanya habari za kipindi chake.
 Bi. Aida Issa akiwa ofisini kwake.
Binj Murithi akinikumbusha enzi za akina Mshindo Mkeyenge. Picha zote na Vijimambo Blog.

No comments: