Advertisements

Wednesday, July 17, 2019

OBITUARY YA BIBI NYAMWELA


BY MOHAMED MATOPE

Bibi yetu Nyamwela amefariki dunia leo tareha 15/7/19, saa moja na nusu, nyumbani kwa mwanawe , Tatu Matope Tabata ,Dar-es-salaam . Amefariki peacefully akiwa amezungukwa na mwanawe, mkwewe na wajukuu zake. Akanyamwela alikuwa na umri wa miaka inayokadiriwa kuwa 105-110.

Tutamkumbuka Akanyamwela kwa moyo wake wa genorocity, moyo wa kugawa) ,hakuwa tajiri , hakuwa na mali , lakini alikuwa na moyo wa kutoa kile kidogo alicho nacho. Nakumbuka wakati tupo watoto , ilikuwa kila tukienda kumtembelea nyumbani kwake Utete, alikuwa anatumia usiku mzima kututengenezea pepeta za kula na kubeba wakati wa kurudi Dar. Anatupikia wali wa mpunga mpya na njambu(kisamvu) cha mbaazi ,(na alikuwa mpishi mzuri sana) tunakula mapaka tunaacha , na bado atahakikisha anatufungia chakula kingine cha kurudi nacho Dar. Akanyamwela alikuwa ni mchumi mkubwa, alitumia kile kidogo alichonacho kuhakikisha watoto na wajukuu zake wanaishi maisha mazuri. Nyumba yake ilikuwa ni mahali pa wajukuu na vijana tofauti kijijini, kusimama na kula chakula . Jiko lake lilikuwa na chakula muda wote.

Labda Legacy yake kubwa ni alikuwa independent woman. Alishawahi kuolewa mara mbili,na baada ya hapo aliishi kama single mother zaidi ya nusu ya maisha yake. Lakini aliweza ku manage maisha yake , ya watoto na wajukuu, kwa income yake mwenyewe in large part, ilitoka kwenye shamba lake la mpunga na mahindi. Mimi binafsi sijawahi msikia Akanyamwela akiniomba msaada wowote direct or indirect katika uhai wake. Hakuna kitu kilichokuwa kinamkera moyoni kwake, kama kuishi juu ya mgongo wa mtu ,hata kama kwenye mgongo wa mtoto wake mwenyewe aliyemzaa. Mpaka akiwa yupo kitandani , hawezi hata kusimama , miezi michache iliyopita, bado alikuwa anawalazimisha wazee , wamrudishe nyumbani kwake Utete .

Alikuwa sio mtu wa kulalamika . Pamoja na kuwa katika maisha yake amepatwa na mikasa na mitihani mingi , sijawahi kumsikia aki complain. Katika uhai wake amezika 2 ex-husbands wake, babu Mahimbwa na Mzee Mbonde, watoto wake wote watatu wa kiume , Saidi, Shamte na Masudi, lakini hatujawahi kusikia akimlalamikia Mungu , yeye aliendelea kudunda na maisha yake.

Alikuwa family woman, mtu anayejali familia , watoto wake hata baada ya kuwa watu wazima , kwake yeye bado aliwaona kama watoto wachanga , na hakuwahi kulikwepa jukumu lake kama mama mzazi. Alimlea Mjomba Saidi , first born wake in his 60’s , wakati akiwa mgonjwa kitandani ( yeye akiwa na umri wa zaidi ya miaka 90) alimwogesha ,alimlisha , alimbadirisha nguo, mpaka siku ya umauti wake. Akanyamwela ametulea sisi wajukuu zake wote kwa upendo mkubwa katika utoto wetu.

Tunauhakika kuwa mama yetu amefarijika sana kwa kuwa na mama mwenye roho nzuri kama Akanyamwela. Na vilivile mama amefarijika kwa kurudisha fadhila ya kumlea mama yake katika uzee wake mpaka siku hii ya leo alipofariki. Sisi kama wajukuu tunamshukuru mungu kwa kutupa muda mrefu wa kuishi na mwanamke jasiri , Bibi Nyamwela.

Ukweli ni kuwa siku hii ya leo tunasherehekea maisha ya Akanyamwela na kumshukuru mungu kwa kumpa zawadi ya kushuhudia majanga mengi hapa ulimwenguni . Katika uhai wake Akanyamwela amaeona , vita kuu ya kwanza ya dunia , great depression ya mwaka 1933, 19th amendment in USA constitution ( sheria iliyoruhusu wanawake kuanza kuvoti ), maraisi 19 wa USA, assassination za President Kennedy, Martin Luther King na Bob Kennedy ,Mkoloni Mjerumani, Mwingereza, 2 world war ,uhuru , 5 TZ presidents, 21 USA presidents, Jim Crow rule,, Brown v Board of education 1948 (case iliyoruhusu blacks wachanganyike na wazungu mashuleni) , voting rights act ya 1963( act iliyowapa black haki ya ku voti) , case ya Virginia V love ya mwaka 1963 ( kesi iliyo allow interracial marriage kati ya back na white) , Rosa Park revolt in 1958, Montgomery bus boycott 1959, (movement iliyoruhusu blacks kukaa kwenye viti vya mabasi pamoja na whites) na mwisho ameshuhudia USA ikimchagua raisi wa kwanza black , Baraka Obama. Akanyamwela ameacha mtoto mmoja , mama yetu , wajukuu 30 na vitukuu 55.

No comments: