Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja na mlalamikaji alipe gharama za kesi.
Kwa sasa, mchakato ya kuichilia ndege hiyo kurejea nchini ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg inaendelea.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo huko mahakamani amesema kuwa Tanzaia imeridhishwa na uamuzi wa mahakama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dkt. Ndumbaro akitoa maelezo kuhusu kuachiwa kwa Ndege ya Tanzania, iliyokuwa imeshikiliwa nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment