ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 5, 2020

DC MGEMA ATOA BAISKELI KWA WALEMAVU

Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema akimkabidhi mkazi wa mtaa wa Bombambili katika Manispaa ya Songea Frowin Fungo ambaye ni mlemavu wa miguu fedha taslimu shilingi laki 1 ili ziweze kumsaidia kuongeza mtaji katika shughuli zake za kushona viatu ambapo pia alimpa Baiskeli ya magurudumu matatu ambayo itamwezesha kutoka nyumbani na kwenda katika shughuli zake.
Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema kushoto akimsikiliza mkazi wa kijiji cha Mpitimbi Aron Ponera anayejishughulisha na kilimo baada ya kumpa baiskeli ya magurudumu matatu itakayomwezesha kwenda na kurudi shambani,
Ponera licha ya ulemavu wake lakini amekuwa akijishughulisha na kilimo kwa ajili ya familia.

Picha zote na Muhidin Amri


Na Muhidin Amri,
Songea

MKUU wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema,amewataka vijana wilayani humo kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili iwe rahisi kwa serikali kupitia halmashauri za wilaya kuwapa mikopo isio na riba ambayo itawawezesha kuanzisha vikundi vya kiuchumi na kujikwamua na umaskini.

Amesema hayo jana wakati akikabidhi msaada wa baiskeli ya magurudumu matatu na fedha shilingi laki moja kwa mkazi wa mtaa wa Bombambili manispaa ya Songea Frowin Fungo ambaye ni mlemavu wa miguu anayejishuhulisha kushona na kung’arisha viatu katika kituo cha mabasi cha Mfaranyaki manispaa ya Songea.

Alisema, Fungo amefika ofisi ya mkuu wa wilaya mara tatu kuomba fedha ili aongeze mtaji wake, kwa hiyo aliwasilina na wadau kwa ajili ya kupata baiskeli ambayo itamsaidia kwenda na kurudi katika shughuli zake za kila siku.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya, Fungo amepata msaada wa baiskeli na fedha hizo kutokana na yeye mwenyewe kuanza kuchukua hatua na kuanzisha shughuli ambayo ina muingizia kipato kinachomsaidia kuendesha maisha yake licha ya ulemavu alionao badala ya kukaa barabarani na kuomba omba kwa wapiti njia.

Alisema, kama walemavu na vijana wakiungana pamoja itakuwa rahisi kwa halma

No comments: