Mkurugenzi wa mipango, ufatiliaji na tathmini wa tume ya Taifa ya uchaguzi Adam Mkina wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RAS Kagera octoba 05, mwaka huu Bukoba Manispaa.
Mratibu wa uchaguzi mkoa wa Kagera Mapinduzi Serian akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbaliya uchaguzi kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi ulioandaliwa na ume ya Taifa ya uchaguzi.
Sheikh wa mkoa Kagera Alhaji Kharuna Kichwabuta aliyesimama akiomba dua ya ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi ulioandaliwa na tume ya Taifa ya uchaguzi manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Na Allawi Kaboyo – Bukoba.
Wakati vyama vya siasa nchini vikiendelea na zoezi la kuomba kuchaguliwa na wananchi kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Tume ya uchaguzi NEC ivitahadharisha vyama hivyo kutofunja dheria za nchi kwa kigezo cha uchaguzi.
Katika hotuba ya mwenyekiti wa NEC iliyosomwa na mkurugenzi wa mipango, ufatiliaji na tathmini wa tume ya Taifa ya uchaguzi Adam Mkina wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Kagera uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa RAS Kagera octoba 05, mwaka huu, ameeleza kuwa pamoja na masuala yote ya uchaguzi suala la utulivu na amani vinatakiwa kupewa kipaumbele.
Amesema kuwa Tume imekuwa ikisisitiza umuhimu wa vyama vya siasa na wagombea kuzingatia maadili ya uchaguzi katika kampeini zao, ikiwemo kuepuka lugha za kashfa maneno ya uchochezi yanayotishia amani na usalama wa nchi pamoja na kuhakikisha wanaepuka kufanya kampeini ambazo zinaashiria ubaguzi katika misingi ya jinsia, ulemavu, ukabila, udini, maumbile au Rangi.
“Tunaendelea kuwasisitiza vyama na wagombea kuwa kunapokuwa na malalamiko yoyote ya kimaadili basi hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo,kuwasilisha malalamiko kwenye kamati za maadili ndani ya muda uliyowekwa na sio kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.” Amesisitiza Adam
Mkina ameongeza kuwa tume inaendelea kuratibu kusimamia na kuendesha uchaguzi huu kwa kutumia sheria za uchaguzi, ambapo amesisitiza kuwa vyama vya siasa wagombea na wananchi wanakumbushwa kuwa katika kipindi hiki, sheria nyingine za nchi hazijasimama hivyo wajihadhari na vitendo ama mattamshi ambayo yanaweza sababisha vurugu kwa kisingizio cha uchaguzi.
Aidha ameongeza kuwa katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura umewezesha daftari hilo kuwa na jumla ya wapiga kura 29,188,347 nchi nzima, ambapo pia wagombea kutoka vyama vya siasa 15 waliteuliwa na kugombea nafasi za urais huku wawili kati yao wakiwa wanawake pamoja na wanawake 5 kuteuliwa kuwa wagombea wenza.
Kwaupandewake Msimamizi wa uchaguzi manispaa ya Bukoba ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo amewahakikishia wananchi wa manispaa hiyo kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki hivyo wanao wajibu wa kujiokeza kupiga kura kwaajili ya viongozi wanaowataka.
Mkutano huo umewakutanisha wadau ambao ni waandishi wa habari, vongozi wa dini, asasi za kiraia, watu wenye ulemavu na mashirika mbalimbali yanayojihusisha na elimu ya mpiga kura.
No comments:
Post a Comment