Advertisements

Friday, December 4, 2020

SERIKALI YAIMARISHA MIFUMO YA UKUSANYAJI WA MIRAHABA YA KAZI YA WASANII

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi namna serikali imeboresha kanuni za ukusanyaji wa mirabaha ya kazi za wasanii , leo Desemba 3, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na Watayarishaji wa kazi za Muziki na Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s katika mkutano wa kujadli namna bora yakuisaiida sekta ya sanaa ili iweze kukua na kuendelea kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya kuendeleza sekta ya Sanaa.
Mtayarisha wa kazi za Filamu nchini William Mtitu akimuomba Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) kusaidia kupunguza utitiri wa kodi katika vifaa vya kuandalia filamu pamoja na makato ya kodi kwa kazi wanazozalisha, leo Desemba 03, 2020 Jijini Dar es Salaam, katika mkutano na Watayarishaji wa kazi za Muziki na Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s, wa kujadili namna bora yakuisaiida sekta ya sanaa ili iweze kukua na kuendelea kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya kuendeleza sekta ya Sanaa.
Mwongozaji wa Sanaa za Maaonesho Bw. M Mwamnyenyerwa akiiomba serikali kujenga kumbi za kufanyia sanaa za maonesho katika kila mkoa ili kuendeleza sanaa hiyo inayoonekani kuanza kupotea nchini, leo Desemba 03, 2020, katika mkutano na Watayarishaji wa kazi za Muziki na Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s, wa kujadili namna bora yakuisaiida sekta ya sanaa ili iweze kukua na kuendelea kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya kuendeleza sekta ya Sanaa.
Baadhi ya Watayarishaji wa kazi za Muziki na Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi aliyeketi (watatu kushoto) leo Desemba 03, 2020 Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kumaliza mkutano na Watayarishaji wa kazi za Muziki, Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s, wa kujadili namna bora yakuisaiida sekta ya sanaa ili iweze kukua na kuendelea kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya kuendeleza sekta ya Sanaa.
Dj Mkongwe Boniface Kilosa maarufu kama ‘DJ LOVE’ akiiomba serikali kuboresha mitaala ya elimu ya msingi katika masuala ya sanaa ili Sanaa iweze kuwa sehemu ya maisha ya watoto na kutambua vipaji vyao mapema, leo Desemba 03, 2020, katika mkutano na Watayarishaji wa kazi za Muziki na Filamu,Waongozaji wa Filamu na MaDJ’s, uliyofanyika Jijini Dar es Salaam kujadili namna bora yakusaidia sekta ya sanaa iweze kukua na kuendelea kufuatia ahadi ya Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ya kuendeleza sekta ya Sanaa.wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza na wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Emmanuel Ishengoma.

Na Anitha Jonas – WHUSM, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali amesema kuwa tangu COSOTA ihamie wizara hiyo imeboresha Kanuni mbalimbali ambazo zitasaidia kuongeza ukusanyaji wa mirabaha na imeongeza adhabu ya faini kutoka milioni 5 mpaka milioni 20 kwa mtu anayekamatwa na uharamia wa kazi za Sanaa, pia Kanuni hizo zimetoa nafasi ya Mtendaji wa COSOTA kuwa na mamlaka ya kutoza faini hiyo papo kwa papo.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Desemba 03, 2020 Jijini Dar es Salaam katika mwendelezo wa mikutano yake ya kukutana na makundi mbalimbali ya Sanaa, ambapo kwa siku hii alikutana na MaDJ’s, Wataarishaji wa Muziki na Filamu na Waongozaji wa Filamu.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Dkt.Abbasi alitoa msisitizo kwa BASATA na Bodi ya Filamu kuweka juhudi zaidi katika kujenga sekta ya Sanaa badala ya kudhibiti au kufungia.

“Serikali kwa sasa ipo katika hatua za kuboresha mifumo ya hakimiliki ili kuhakikisha wasanii wa makundi yote wananufaika na ubunifu wa kazi zao kwa kila zinapotumika katika mazingira yoyote hivyo basi ni muhimu kwa kila msanii kusajili kazi yake ili aweze kunufaika na kwa upande wa waandaaji wa muziki ni vyema wakafahamu umuhimu wa kuwa na umiliki wa midundo ‘beats’ wanazoandaa na kusajili,”alisema Dkt. Abbasi.

Pamoja na hayo naye Mtendaji Mkuu wa COSOTA Doreen Sinare aliwasihi Watayarishaji wa kazi za Muziki kusajili kazi zao kwani hawawezi kupata haki zao kama hawatasajili ‘beats’ wanazoandaa, ambapo alifafanua mara nyingi imekuwa ikionekana kama Mwanamuziki ndiyo mwenye umiliki wa kila kitu katika muziki na ubunifu wa mtayarishai huyo kusahaulika.

Halikadhalika katika mkutano huo Dkt. Abbasi aliwasihi wadau wa Sanaa kuanisha utitiri wa kodi zinazosumbua sekta hiyo ili serikalini iweza kujenga hoja ya namna zinaweza kupunguzwa,pia aliwasihi wasanii hao kuanisha mahitaji ya mafunzo yatakayowasaidia kuongeza ufanisi katika kutekeleza kazi zao kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)

No comments: