Advertisements

Monday, January 18, 2021

DKT.TULIA ASHUSHA MILION 60 UJENZI WA SHULE MBEYA

  
Mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amefanya ziara katika shule ya Sekondary Iduda iliyopo mkoani Mbeya ambapo amekabidhi jumla ya Shilingi Milioni sitini, laki tano na sabini na nne elfu (60,574,000/-) ambazo ni fedha zote za mfuko wa maendeleo wa jimbo hilo wa mwaka wa fedha 2020-21 ili kusaidia ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika Shule hiyo.

Dr. Tulia amesema>>>”Kama tunavyofahamu kwamba Wilaya yetu imekuwa na uhaba mkubwa wa shule za Sekondari zenye kidato cha tano na sita na zaidi katika bonde letu la Uyole hakuna hata shule moja hivyo basi leo hii tumekuja hapa baada ya kukubaliana kwamba fedha zote za mfuko wa Jimbo zitaelekezwa hapa Iduda kwa ajili ya ujenzi wa shule”

“Fedha hizo tulizozitoa zinao uwezo wa kujenga madarasa matatu ambayo tutaanza nayo na huo ujenzi utaanza mara moja kwa sababu fedha zipo, Mbeya mjini safari hii tunahitaji maendeleo na hatutarajii kuona mtu wa kutukwamisha. Ndugu zangu niwaombe sana, fedha hizi hazitatosheleza kujenga na kufikia mahitaji yetu yote kwasababu bado tutahitaji pia mabweni hivyo basi tunapaswa kushirikiana kwa umoja wetu kila mmoja anapoweza hata kutoa nguvu kazi ikiwemo kuleta mawe n.k”-Dr. Tulia Ackson

“Safari hii mtoto aliyeongoza kidato cha nne ametoka hapahapa Mbeya hivyo basi tunataka tuendelee kuweka mazingira mazuri ili kuongeza ushindani mzuri zaidi katika siku za usoni na ikibidi Mbeya tuendelee kuwa vinala wa elimu nchini”- Dr. Tulia Ackson

No comments: